BongoCelebrity

IDDI SIMBA KIZIMBANI:TAFSIRI YA MAGGID MJENGWA
Ndugu zangu,

Nimeiona habari kubwa kwenye ITV usiku wa leo; Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw. Iddi Simba amefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.  Ni Iddi Simba ambaye alilazimika kujiuzuru uwaziri kwa kashfa ya sukari. Ni Iddi Simba ambaye huko nyuma aliipigania sana sera ya Uzawa.

Na kadhia iliyomkumba sasa  inahusu kafsha ya UDA. Ni  lililokuwa Shirika la Usafiri Dar Es Salaam. Iddi Simba amesomewa mashtaka 8 ikituhumiwa   kudanganya, kughushi na kulitia hasara ya shilingi milioni  320 Shirika la Usafiri Dar es Salaam ( UDA).

Tafsiri yangu;

Huu ni mwendelezo wa mwanzo uliotiliwa mashaka. Kuna watakaoanza kuamini, kuwa zama za kulindana zimeanza kufikia ukingoni.

Iddi Simba ni kigogo. Ni Mzee wa Dar es Salaam. Ni Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es Salaam. Leo amefikishwa kwenye Mahakama ya katikati ya Jiji la Dar. Bila shaka, kuna ambao hawakuamini kumwona Idi Simba kwenye runinga akikalia kwenye benchi la Mahakamani.

Naam, tunaziona ishara la wimbi kubwa linalokuja, si dogo hata kidogo. Yumkini naye anasafisha njia ya wengine kufuatia. Na tusubiri tuone.

Maggid Mjengwa

Iringa

http://mjengwablog.com

JINSI YA KUTUMIA TWITTER ILI KUKUZA/KUTANGAZA BIASHARA YAKO
Makampuni mengi siku hizi yanatumia mtandao jamii wa Twitter kwa minajili ya kutangaza biashara zao na hivyo kuongeza kiwango cha mauzo yao kwa kupata au kuvutia wateja wengi zaidi.  Ukikuta kampuni au biashara haiutumii mtandao wa Twitter kwa kuwasiliana na wateja waliopo na wa mbeleni,basi tambua kwamba kampuni hiyo haiendi na wakati. Yaweza kuwa kwa makusudi au kwa kutokutambua tu faida zilizopo katika matumizi ya Twitter na hata mitandao mingine ya kijamii(Social Networks).

Pamoja na kuzidisha matumizi ya Twitter, yapo makampuni, makubwa kwa madogo, ambayo bado wanashangaa kwamba inakuwaje watu wanaowafuata(Followers) hawajaweza bado kubadilika na kuwa zaidi ya wafuatiliaji tu na badala yake  kuwa wanunuzi wa bidhaa au huduma. Kwanini?

Ni wazi na ukweli kwamba Twitter ni sehemu nzuri ya kutangazia biashara, matukio, kampeni za kusaidiana(kuchangishana fedha na mambo kama hayo) achilia mbali sehemu nzuri ya kupashana habari,kuelimika na kuburudisha kama ambavyo niliwahi kuandika katika post hii hapa.

Lakini kuandika tu (Tweets) haitoshi kukusaidia kukuza biashara kwa maana ya kuongeza wateja na kipato. Unahitaji uelewa wa ndani zaidi juu ya hadhira yako(audience), uwe na mpango thabiti wa mitandao jamii na uwe na njia mahususi ya kupima mafanikio yako kupitia Twitter. Muhimu zaidi unahitaji kujua jinsi gani na kwa namna gani utatumia Twitter kabla hujaanza. Haya hapa ni mambo machache unayoweza kuzingatia;

Fanya Utafiti: Utafiti kuhusu soko lako(Market Research) ni kitu cha lazima endapo unataka kuongeza nafasi za mafanikio yako. Kuuliza maswali muhimu na yanayoeleweka kwa jamii ya Twitter ni njia nzuri na rahisi ya kuelewa kwa undani kuhusu yaliyo muhimu kwa wateja wako.Wanataka nini? Ni kitu gani wanakitazamia kutoka kwako au kwa biashara yako.Ni aina gani za huduma ambazo wanazipendelea zaidi kutoka katika biashara yako? Ni kitu au vitu gani vinavyochangia maamuzi yao ya kutumia au kuchagua huduma au bidhaa kutoka kwako? Wanasemaje au wana maoni gani kuhusu washindani wako wa biashara.

Ukitenga muda maalumu wa ku-tweet kwa minajili ya kupata undani wa soko, bila shaka wateja wako, wa sasa na hata wa baadae, watakuchukulia kama mtu ambaye unaingilika, unasikiliza na wanaweza wakajisikia huru zaidi kutumia huduma au bidhaa kutoka kwako.Unakuwa karibu zaidi nao na unawajali.

Kuwa na Mpango/Mbinu Maalumu: Biashara za aina zote, zinahitaji kuwa na mpango maalumu wa kuwapata wateja, kubakia nao na kujenga  msingi imara wa wateja hao kitu ambacho ni muhimu sana kwa maendeleo ya kweli ya biashara. Pamoja na njia zote za matangazo bado neno la kuambiwa kutoka kinywani kwa mtu mwingine(word of mouth) lina maana zaidi.Huo ni msingi.

Kwa hiyo kabla ya kuanza ku-tweet, jaribu kwanza kufanya utafiti kuhusiana na jamii yako ya mtandaoni(online community) na jinsi gani ujiingize au ushiriki katika jamii hiyo ukiwa miongoni mwao. Weka mpango madhubuti wa jinsi utakavyokuwa ukituma au ku-post tweet zako, mara ngapi utakuwa unafanya hivyo bila kusahau kuzingatia utakachokuwa una-post.

Muhimu zaidi hapa ni kuzingatia je hiki ninacho-post kitaamsha hisia za mtu kubofya(kama umeweka link kwa mfano), na je hii Tweet yangu itaongeza uelewa kwa wateja wangu,wa sasa na wa baadae, juu ya aina au huduma tunazotoa? Je, tweet hii itapelekea kuongezeka kwa masoko? Kwa tweet hii,wateja zaidi watashawishika kutumia bidhaa au huduma zinazotolewa na biashara yangu? Hayo ni baadhi ya maswali muhimu ya kujiuliza

Hakikisha wateja wanaelewa undani wa Bidhaa/Huduma zako: Kabla biashara yako haijaanza kutengeneza pesa, inahitaji kujenga kitu kinachoitwa social media magnetism. Hii tunaweza kusema ni sumaku ya/ndani ya mitandao jamii. Cha kwanza kufanya hapa ni kutumia watu unaojuana nao au ambao wanajua kuhusu biashara yako(watu wako wa karibu na watu unaokutana nao ana kwa ana wanafaa sana hapa) kwa ajili ya kuitambulisha biashara yako na kuwashawishi wengine watue kwenye ukurasa wako wa Twitter na hivyo wafuate brand yako.

Hapa ndipo panapokuwa na umuhimu wa kutumia jina linakubalika au kutambulika kirahisi.Kuwa na logo na kuitumia hiyo logo katika kila kitu kinachohusiana na biashara yako.Hakikisha kwamba ukurasa wako wa Twitter,unatambulika hivyo kwanza.

Kisha wafuate(Follow) wataalamu au wazoefu wengine katika aina ya biashara unayofanya. Yafuate makampuni mengine, wafuate washindani wako wa kibiashara.  Changia mawazo hususani kuhusu utaalamu ulionao ili kuongeza heshima yako katika sekta. Kwa kufanya hivyo pia utakuwa unaongeza imani miongoni mwa wateja wako.Watakukubali zaidi. Chagua aina mahususi ya kushiriki katika mijadala mbalimbali kuhusiana na sekta au aina yako ya biashara.Chagua “sauti” ambayo itakuwa ni rahisi kwa watu kutambua.Ninaposema sauti ninamaanisha aina ya ujibuji maswali au uchangiaji.

Shirikisha Wateja Wako: Miongoni mwa makosa makubwa ambayo wamiliki wa biashara wanayoyafanya ni kutokuwa karibu na wateja wao. Ninapoongelea kuwashirikisha wateja wako ninamaanisha kuwa karibu nao.Kuwasikiliza kwa makini juu ya malalamiko,matarajio yao nk. Mitandao jamii ni sehemu nzuri ya mazungumzo au mijadala. Kwa maana hiyo, usiache kuwajibu wateja wako hususani katika zile Tweets ambazo zinaitaja au kuhitaji majibu kutoka kwako. Anzisha mazungumzo na pia shiriki mazungumzo. Katika mazungumzo hayo kuwa mkweli,muaminifu na utoe habari au taarifa ambazo zimefanyiwa utafiti.Usikurupuke.

Wajali wafuasi wako: Kadiri wateja wanavyozidi kuwa wengi,(hususani kwa makampuni au biashara ndogo ndogo) uwepo wako mtandaoni unaweza kupungua kwa kisingizio cha kuwa “busy”.Usifanye hilo kosa. Hakikisha kwamba unaendelea kuwepo mtandaoni.Hakikisha kwamba unaendelea kufanya yote niliyoyataja hapo juu ikiwemo kushiriki mijadala, kuuliza maswali ili kupata undani wa soko, kushughulikia malalamiko nk. Biashara nyingi zimekuwa zikitumia Twitter kama chombo cha kuhakikisha kwamba wateja wanaendelea kutumia bidhaa au huduma zao.

Tumia pia fursa hii kuwajulisha wateja wako kuhusiana na kile kinachoendelea katika sehemu yako ya biashara. Kama utakuwa umefunga kwa sababu moja au nyingine, waambie.Kama una punguzo la bei kwa bidhaa au huduma,waambie. Washirikishe kwa kila namna.Kwa kufanya hivyo kwanza hawatokusahau na pia wataona ni jinsi gani unavyowajali. Kila la kheri katika biashara yako.

Jeff Msangi ni Mhariri Mkuu wa www.bongocelebrity.com. Unaweza kuwasiliana naye kupitia jeffmsangi at gmail.com au jeffmsangi at bongocelebrity.com

MKASI-SO2E15 WITH ENTERTAINERS JOSE MARA,LILIAN INTERNET AND SUPER NYAMWELA
Katika kipindi cha Mkasi cha wiki iliyopita, ilikuwa ni zamu ya Jose Mara,Lilian Internet na Super Nyamwela ambao majina yao sio mageni kabisa katika ulimwengu wa burudani nchini Tanzania. Wasikilize walivyoambaa na Salama Jabir

HOTUBA YA NAIBU KATIBU MKUU CHADEMA,MH.ZITTO KABWE KWA WANA-CHADEMA NA WATANZANIA NCHINI MAREKANI
Tumekutana leo wakati ambao Taifa letu lipo katika mpito wa mambo mengi sana.

Kufuatia shinikizo kubwa kutoka chama chetu cha CHADEMA na asasi nyingine za kiraia ikiwemo viongozi wa dini, tupo katika mchakato wa kuandika upya katiba ya nchi yetu. Lakini pia kuna muamko mkubwa sana wa haki za kiraia na haki za kisiasa katika Taifa letu hivi sasa. Watanzania, kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi yetu, wameamka na kutaka mabadiliko ya kisiasa na hasa kutaka kabisa uongozi mpya wa nchi kutoka chama kingine tofauti na chama kinachoongoza hivi sasa. Huu mpito pia, Mpito wa kutoka chama kimoja hodhi kwenda mfumo wa kweli wa vyama vingi vya siasa. Watanzania wameamka sana kujua rasilimali za nchi yao na kutaka kutokomeza rushwa na ufisadi na matumizi mabaya ya utajiri wa nchi. Huu ni mpito wa kutoka viongozi wanaojali maslahi yao binafsi na kwenda kwa viongozi wawajibikaji na wenye uchungu wa kuendeleza nchi yetu na watu wake.

Mpito wowote unapaswa kuongozwa vyema. Unapaswa kushirikisha wananchi wote bila kujali wapo sehemu gani ya Dunia. Chama chetu kipo mstari wa mbele kuongoza mpito tulionao Tanzania. Licha ya kuongoza juhudi za kuwa na Katiba mpya itakayohakikisha HAKI na Wajibu wa Watanzania, lakini pia tumekuwa tukiendelea kupambana na rushwa na ufisadi. Pia tumekuwa tukiendelea kuhakikisha utajiri wa nchi  yetu unatumika kwa manufaa ya Watanzania. Hatujatetereka hata kidogo na hatutateterekea kuhakikisha Watanzania wanakuwa na Taifa lenye demokrasia iliyokomaa, lenye maendeleo na ustawi wa watu wake (Developmental Democratic State).

Licha ya kwamba tupo Upinzani, lakini hatua mbalimbali tulizochukua zimeleta mabadiliko makubwa katika nchi yetu. Kuanzia vuguvugu la Buzwagi mpaka kuibuliwa kwa maskandali ya EPA na mpaka kutajwa kwa orodha ya Mafisadi nchini pale MwembeYanga. Hata hivi karibuni juhudi za Bunge kutaka Uwajibikaji Serikalini zilizoongozwa na CHADEMA zimeleta mabadiliko. Inawezekana mabadiliko hayo sio kama tutakavyo, sio kamili, lakini ni hatua ambayo tumepiga. Tutaendelea kama chama cha siasa sio tu kusema na kupiga kelele kuhusu uoza uanaofanyika Serikalini (maana ndio kazi yetu kikanuni) lakini pia kutoa masuluhisho ya matatizo ya nchi yetu na kusukuma kupitia Bunge mabadiliko chanya yanayotakiwa ili kuleta mabadiliko nchini.

Ni matumaini yangu kwamba Watanzania wanaoishi nje ya nchi, kokote walipo watashiriki pamoja nasi katika vuguvugu (movement) hili la kuleta mabadiliko katika Taifa letu. Hampaswi kukaa na kutazama, bali mnapaswa kushiriki kikamilifu maana hii ni nchi yetu sote. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha nchi yetu inakuwa na demokrasia na ustawi wa watu wake.

Hali ya Uchumi wa Nchi

Tumekuwa moja ya nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi duniani. Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa wastani wa asilimia 6. Kazi hii ya ukuaji ukilinganisha na kiwango cha ukuaji wa idadi ya watu (ambacho ni 2.8%) ingeweza kupunguza umasikini kwa zaidi ya 50% katika kipindi hicho. Hata hivyo Umasikini Tanzania umebakia ni mkubwa ambapo zaidi ya Watanzania 37 katika kila Watanzania 100 hawana uhakika wa mlo mmoja kwa siku.

Idadi ya Watanzania masikini wa kutupwa (wenye kipato cha chini ya tshs 500 kwa siku) imeongezeka kutoka watu milioni 12 mwaka 2007 mpaka watu milioni 15 mwaka 2011. Ukitaka kujua wingi huu ni wa kiwango gani, chukua idadi ya watu wa Nchi ya Botwasana, Namibia, Swaziland na Lesotho haikaribii idadi ya Watanzania wenye mashaka ya mlo mmoja kwa siku. Idadi ya watu wa Denmark, Netherlands, Norway na Uholanzi kwa pamoja ndio sawa na idadi ya Watanzania masikini. Kwa nini?

Ni kitendawili. Ni nadra kukuta uchumi unaokua kwa kasi kama wetu ukizalisha masikini  zaidi. It’s a paradox of a fast growing economy and increasing poverty. Kwa miaka kumi ambayo tumeiangalia (2000 – 2010) tumeshuhudia kwa dhahiri kabisa kushindwa kwa sera za kuondoa umasikini zinazotekelezwa na Serikali ya CCM.

Masikini wa Tanzania wapo vijijini zaidi. Uchumi wa vijijini kwa kipindi cha muongo mmoja umekua kwa wastani wa asilimia moja tu. Flat lining. Kwa hiyo uchumi unaokua hivi sasa sio uchumi wa Watanzania bali ni uchumi wa watu wachache kwenye sekta chache kama madini, mawasiliano na ujenzi. Watanzania walio wengi walioko vijijini wanaendelea kuandamwa na ufukara bila juhudi mahususi za kuwasaidia. Tumesema na tunarudia kusema kwamba ni lazima kubadili mwelekeo wa mipango yetu na kujikita kwenye maendeleo vijijini. Kama chama tunaendelea kusema jambo hili ndani ya Bunge na pia kuwaelimisha wananchi kwenye mikutano yetu ya hadhara.

Mfumuko wa Bei umefikia kiwango cha juu sana cha 19% na hivyo hata mikopo katika mabenki imekuwa ghali hadi kufikia riba ya 23% na zaidi. Mfumuko wa bei unaongozwa na bei ya vyakula. Katika hali ya kawaida, kupanda kwa bei za vyakula kungemnufaisha mkulima lakini hali sio hiyo Tanzania. Mkulima bado anauza mazao yake kwa bei za vijijini ambazo ni ndogo na zinaamuliwa na wachuuzi wa mijini. Lakini mkulima huyu anaponunua bidhaa za matumizi yake kama sukari, mafuta ya taa, nguo nk ananunua kwa bei za mijini ambazo zimeathiriwa vikali na mfumuko wa bei. Hivyo mfumuko wa Bei unamuathiri zaidi mwananchi masikini kabisa. Serikali imekuwa mlalamikaji kama wananchi wengine. Mfumuko wa Bei utapungua kwa kuongeza uzalishaji wa chakula, kuimarisha miundombinu ya vijijini na kupunguza gharama za Nishati kama hasa Umeme. CHADEMA inaendelea kuisukuma Serikali kuchukua hatua ili kupunguza makali ya maisha kwa wananchi. Hatua za muda mfupi zihusishe nafuu ya kodi kwenye bidhaa zinazotumiwa na wananchi kwa wingi.

Hata hivyo bado matumizi ya Serikali ni makubwa mno kwenye masuala ambayo hayana uhusiano na kuendeleza watu. Bado bajeti ya posho mbalimbali, safari za nje na hata matumizi makubwa ya magari ya serikali ni kubwa mno kulinganisha na hali yetu ilivyo. Katika matumizi haya pia kuna ufisadi mkubwa sana. CHADEMA inaendelea kuanisha masuala haya na kukemea na kuchukua hatua pale inapobidi.

Uwezo wetu wa kukusanya mapato ni changamoto kubwa. Mapato mengi yanapotea kama misamaha ya kodi ambayo sasa imefikia tshs 1.3trn kwa mwaka. Mapato mengine hayakusanywi kwa sababu ya ukwepaji kodi uliokithiri. Kodi kwenye Sekta ya Madini imekuwa ni mjadala wa muda mrefu sana. Sheria ya madini ya mwaka 1998 na Sheria za Fedha ya mwaka 1997 ziliweka mfumo wa kinyonyaji kabisa ambao ulikuwa unafaidisha makampuni ya uchimbaji madini kuliko Taifa. Sheria mpya ya madini ya mwaka 2010 ambayo ilitokana na kazi kubwa tuliyofanya ndani ya Bunge pamoja na Mashirika yasiyo ya kiserikali imeweka mfumo bora zaidi. Hata hivyo makampuni ya Madini yaliweka mgomo kwenye sheria mpya kwa kukataa kuanzisha miradi mipya na hata kukataa kuhamia kwenye sharia mpya. Sheria mpya inataka Serikali kuwa na hisa kwenye kila mgodi, hisa za kampuni za madini kuorodheshwa katika Soko la hisa la Dar es Salaam na kulipwa kwa mrahaba mpya wa asilimia 4 kwa kanuni mpya ya kukokotoa mrahaba (from Netback Value to Gross value) ambayo ingeongeza mapato ya Serikali maradufu. Kwa miaka Serikali imekuwa inapoteza mapato kwa kutotekelezwa kwa sharia mpya. Nimesikia kuanzia mwezi huu kampuni ya Barrick imeanza kulipa mrahaba mpya. Tutataka maelezo ya Serikali kuhusu kampuni nyingine na pia mrahaba wa miaka ya nyuma. Ni lazima Serikali ihakikishe nchi inafaidika na rasilimali zake.

Tunaenda kwenye Uchumi wa Gesi Asilia. Makampuni mawili makubwa duniani yamegundua Gesi Asilia nchini kwa kiwango kikubwa sana. Hivi sasa Tanzania ina Utajiri wa Gesi ulitothibitishwa wa 20TCF na makadirio yanaonyesha kuwa tutafika 85TCF katika kipindi kifupi sana. Bado kuna meneo yanaendelea kufanyiwa utafutaji kutokanana vitalu vilivyogawiwa. Hata hivyo hatuna Sera na Sheria ya kusimamia vema sekta hii na hasa yenye kuhakikisha Uwazi na Uwajibikaji. Hatuna pia Sheria ya kusimamia mapato yanayotokana na Gesi Asilia (Petroleum Revenue Management Act). Hatutaki kurudia makosa yaliyofanyika kwenye sekta ya Madini. Tunataka Gesi Asilia itumike kwa maendeleo ya watu wetu.

Tumependekeza kwamba Vitalu vipya vya kutafuta mafuta visitolewe kwa sasa (moratorium) mpaka hapo Sera mpya, Sheria mpya na mfumo bora wa matumizi ya Fedha zitakazotokana na Mafuta na Gesi ziwepo. Pia shughuli za utafutaji katika vitalu vya sasa zitaongeza thamani ya vitalu vijavyo na hivyo nchi kufaidika zaidi.

Tumependekeza pia kwamba ni lazima kuweka mfumo mzima wa uwazi na uwajibikaji katika sekta ili kujipanga vyema na kuepuka yaliyowakuta wenzetu wenye utajiri kama huu ambao uligeuka balaa. Tatu tumependekeza kusomesha Watanzania kwa ngazi zote. Mafundi mchundo kupitia VETA na Mafundi wa kati kupitia Vyuo vya Ufundi.

Muhimu zaidi tunataka kijengwe Chuo Kikuu kikubwa Mtwara chenye Kampasi Lindi ambacho kitakuwa ni kituo cha kufundisha sio watanzania tu bali Waafrika wengine kuhusiana na masuala haya. Ujenzi wa Chuo Kikuu Mtwara unapaswa kuanza mara moja bila kuchelewa.

Kutokana na uzoefu tuliupata katika sekta ya Madini na kupitisha sharia mbaya Bungeni, tunaona kwamba suala la Gesi tukabe kila mahala ili kuhakikisha nchi inafaidika. Historia inatuonyesha kwamba Nchi nyingi za Kiafrika zenye utajiri wa Gesi  na Mafuta hazina demokrasia, zimegubikwa na uvundo wa ufisadi na watu wake ni masikini. Tunataka kuonyesha Dunia kwamba inawezekana kuwa nan chi ya Kiafrika yenye utajiri mkubwa wa Mafuta na Gesi na ikawa ya kidemokrasia, isiyo na ufisadi na yenye watu wenye ustawi. Sio kazi rahisi lakini tumedhamiria. CHADEMA haitakaa tu kuona utajiri wan chi unatapanywa hovyo. Tumesema na kusimamia kwenye Madini, tunatoa mwongozo kwenye Mafuta na Gesi.

Katiba

Ninajua Watanzania mnaoishi nje mna shauku kubwa ya kujua ushiriki wenu na hatma yenu kwenye Katiba mpya. Kwa muda mrefu mmekuwa mkishawishi haki ya kupiga kura, haki ya kuwa na uraia zaidi ya mmoja (Dual Nationality) na hata namna gani mnashiriki katika kujenga uchumi wa nchi.

Kwanza nataka niwapongeze kwa kuchukua uamuzi mzito wa kuondoka nyumbani kuja ughaibuni kutafuta maisha au maarifa au vinginevyo. Nawapongeza zaidi kwa juhudi mnazofanya kusaidia familia zenu nyumbani, vijiji vyenu na hata Taifa kwa ujumla. Takwimu zilizotangazwa na Benki Kuu ya Tanzania zinaonyesha kwamba Watanzania mliopo nje ya Tanzania mlituma nyumbani fedha (remittances) zaidi ya Dola za kimarekani 350 milioni mwaka 2011. Hii ni sawa na asilimia 5 ya mapato yote ya Fedha za kigeni zilizoingia Tanzania mwaka huo na ni zaidi ya Fedha za kigeni zilizoingizwa na Chai, Kahawa, Pamba na Korosho kwa ujumla wake. Kwa hiyo ‘Diaspora’ ni sehemu muhimu sana ya Uchumi wa Taifa ni muhimu Dola iwawekee mazingira mazuri ya kuweza kufanikisha mambo yenu huku ili mshiriki vema maendeleo ya nchi yetu.

CHADEMA tunatambua umuhimu wenu hata kama msingekuwa mnatuma fedha nyumbani. Ninyi ni Watanzania na ni jukumu la Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwalinda popote mlipo duniani. Mtakumbuka mwanzo mwa miaka ya 2000 kulikuwa kuna ‘petition’ ya kudai Uraia wan chi mbili kwa Watanzania. Dkt. Willibrod Slaa alikuwa ni mmoja wa Wabunge waliokuwa wanauliza maswali Bungeni kuhusu jambo hilo. Wengi tuliweka sahihi katika ‘petition’ ile ambayo ilianzishwa na Watanzania wanaoishi nje. CHADEMA inaunga mkono haki ya Watanzania kuwa na uraia wa nchi nyingine. CHADEMA inataka suala hili lifikie mwisho kwenye mjadala wa Katiba. Kuna watu wanasema sio uzalendo Mtanzania kuchukua uraia wa nchi nyingine. Ninasema sio uzalendo pia kuacha raia wako wanateseka nchi nyingine kwa sababu tu wamechukua uraia wa huko au wanashindwa kuchukua uraia wa huko. Sheri zetu za Uraia ni gandamizi hasa kwa wanawake wa Tanzania. Tumepoteza dada zetu wengi  sana na watoto wao kwa sababu wakiolewa na wageni watoto wao hawana haki ya kuwa raia. Wakinyanyaswa na wageni na kutaka kurudi nyumbani wao na watoto wao wananyanyaswa pia kwao. Haikubaliki na tutakabili suala hili kwa nguvu zetu zote. Tunataka Watanzania walioko nje wapate kila aina ya msaada kutoka Dola yetu ili wafanikiwe.

CHADEMA inataka pia Watanzania waliopo nje waruhusiwe kupiga kura nyakati za uchaguzi. Ni suala la ushamba tu kuendelea kujadili jambo hili la uwazi kabisa. Kuna teknolojia za kisasa kabisa kuhakikisha watu wanapiga kura kokote walipo. Mwaka 2004 Chama rafiki cha CHADEMA kutokan Msumbiji RENAMO kiliniteua kuwa wakala wa kura katika kituo cha Ubalozi wa Tanzania Msumbiji uliopo Dar es Salaam. Raia wa Msumbiji wanaoishi Tanzania wanapiga kura nje, seuze Tanzania? CHADEMA  inawahakikishia kulisimamia jambo hili.

Katika mkutano wa Bajeti ujao Bajeti Kivuli itazungumzia namna ya kuimarisha uwekezaji wa Watanzania wanaoishi nje katika uchumi wa nchi. Siku zote tunazungumzia mitaji kutoka nje kwa maana ya ‘Foreign Direct Investments’ peke yake na kwa kweli tunasahau kwamba kuna ‘Diaspora Direct Investments’. Tumetoa vivutio vingi sana kwa Wawekezaji kutoka nje. CHADEMA inakwenda kupendekeza kuwepo kwa vivutio vya kikodi na kirasimu kwa Watanzania wanaoishi nje wanaotaka kuwekeza nyumbani. Ninawashawishi muangalie namna ya kujikusanya na kuwa na ‘Investments Funds’ ili kununua ‘equties’ kwenye miradi mbalimbali. Uwekezaji Tanzania unalipa sana (Return on Investments goes up to 25%) kwenye baadhi ya maeneo. Huduma katika sekta zinazoinukia kama Mafuta na Gesi ni eneo ambalo mnapaswa kuliangalia tusiachie wageni tu. Mnakumbuka wakati wa mwanzo wa Sekta ya Madini hata huduma za kufua nilikuwa zinatolewa na kampuni kutoka Australia! Mtwara hakuna vyumba vya kutosha vya mahoteli na hata nyumba za kupanga, angalieni maeneo haya maana Mtwara is booming. Sisi kama wanasiasa jukumu letu ni kuwawekea mazingira mazuri.

Ninyi mnapaswa kuzileta hizo Dola kidogo mpatazo nyumbani na kuwekeza kwenye maeneo yatakayozalisha ajira na hivyo kuondoa umasikini kwa ndugu zenu. Ninaamini mtachukua changamoto hii na kuangalia namna ya kuitekeleza. Wenzetu kutoka Ethiopia na Kenya wanafanya hivi.

Mjadala wa Katiba pia na hatimaye Katiba mpya itaamua hatma ya Muungano wetu.  Muungano pekee katika Bara la Afrika ambao umedumu na umeonyesha nia ya Mwafrika kukataa mipaka ya kikoloni. Kuna Watu wanaona Muungano huu haina manufaa hivyo uvunjwe. Kuna watu wanaona ni bora kuurekebisha ili uweze kufaidisha Jamhuri mbili zilizoungana. Mchakato wa Katiba mpya kupitia Tume ya Katiba ambayo CHADEMA tumeshiriki, ni nafasi ya kuandaa mustakabali wa Tanzania ijayo. Tanzania tunayoitaka kwa miaka mingine hamsini, mia moja au hata alfu moja. Watanzania wawe huru kusema wanataka Muungano au hawautaki, wanataka Muungano wa namna gani na wanataka Tanzania ya namna gani.

Ni Haki ya Watanzania wanaoishi nje kutoa maoni yao kuhusu Katiba. CHADEMA inakusudia kwanza kukusanya maoni ya wanachama wake walioko nje kuhusu Katiba lakini pia kuitaka Tume ya Jaji Warioba kuja huku kukutana na Watanzania na kupata maoni yao. Ni Haki yenu kutoa maoni na ninawaomba mtumie haki yenu vizuri. Mtupe uzoefu wa nchi nyingine ambazo mmeishi na kuweza kuona ni vipi tutaimarisha Dola imara ya Kidemokrasia yenye kuleta ustawi wa watu wake.

Msimamo wa CHADEMA ni Muungano wa Serikali Tatu. Hata hivyo katika mchakato tulio nao sasa wanachama wa CHADEMA wana uhuru wa kutoa mawazo mapya na kuboresha sera hii ya CHADEMA kuhusu Muungano. Muwe huru kabisa kutoa maoni yenu.

Haki na Wajibu

Watanzania mnaoishi nje mna haki na lazima Dola ilinde haki hizo lakini pia kama Watanzania mna wajibu kwa nchi yenu. Ni wajibu wenu kushiriki kikamilifu katika kuimarisha demokrasia nchini. Sisi wenzenu tumejitoa muhanga katika eneo hili.

Tumejenga taasisi zinazoitwa vyama vya siasa kwa zaidi ya miaka ishirini sasa.

Hatuchoki lakini tunahitaji ushiriki wenu. Jambo hili sio kwa wanachama wa CHADEMA  peke yake bali pia hata wanachama wa vyama vingine mnaoishi hapa Marekani.

Hutakuwa mwanachama bora wa CCM kwa kufanya kazi ya kuwachoma Watanzania wenzako ambao ni wana mageuzi kwa viongozi kila wanapokuja kwenye ziara nje ya nchi. Utakuwa mwanachama mzuri wa chama chako iwapo utawaambia viongozi ukweli wa mambo na namna bora ya kuongoza nchi yetu.

Hamuitendei haki Tanzania kwa kusemana, kusingiziana, kutetana na hata kugombana. Wakati mwingine unapoona mijadala ya watu kwenye mitandao ya kijamii unasinyaa. Unajiuliza sasa kama hawa ndio wapo kwenye mwanga sisi tulio kwenye giza inakuwaje?

Fanya kazi. Furahia maisha. Lakini kumbuka kuna nchi yenye barabara za mashimo, yenye giza muda mwingi wa mwaka kuliko mwanga, yenye umasikini, yenye viongozi wasiwajibika na wala rushwa. Ni nchi yako. Usiseme hii ni kazi ya kina Zitto, Slaa, Mbowe, Nassari, Leticia na Msigwa. Kila mtu ana wajibu wa kufanya kuisogeza mbele nchi yetu. Timiza wajibu wako kwa namna unavyoona inafaa.

Nkrumah once said ‘organise, don’t agonise’ narudia hivyo kwa Watanzania mliopo Marekani. Organise for your motherland.

Tanzania yenye usawa wa fursa

Nimalizie kwa stori yangu. Nilizaliwa katika umasikini wa kutisha kama Watanzania wengi wa vijijini. Nimekwenda shuleni bila viatu na wakati mwingi tumbo likiwa tupu ama nimekunywa uji wa unga wa Yanga uliotiwa chumvi. Darasani nilikuwa ninasoma na watoto wa watu wote wenye mamlaka pale mjini Kigoma. Wote tulikuwa tunafundishwa na Mwalimu huyo huyo na tunakaa darasa hilo hilo, tunapata elimu hiyo hiyo. Leo mimi ni msomi mwenye shahada ya Uzamili na Mbunge nawakilisha watu wa kwetu.

Wenzangu wengi pia wanaendesha maisha yao na wengine wapo hapa Marekani wakitafuta maisha. Leo mtoto wa masikini Tanzania hapati elimu anayopata mtoto wa mwenye uwezo.  Mtoto wa masikini hakutani na mtoto wa mwenye uwezo. Wanasoma shule tofauti. Wanafundishwa na walimu tofauti. Hawachezi pamoja. Wote wakimaliza kidato cha

Sita, mtoto wa mwenye uwezo ana nafasi kubwa zaidi ya kupata mkopo kwenda Chuo Kikuu kwa sababu amesoma shule bora zaidi hivyo anapata daraja kubwa zaidi la kupewa mkopo na Bodi ya Mikopo.

Wakati nasoma, kikwazo kilikuwa uwezo wako tu kichwani. Hivi sasa kikwazo ni kipato pia. Tofauti ya kipato nchini ni kubwa lakini sisi wanasiasa hatuioni. Wakati wenzetu wanajiandaa kufaidika na ‘demographic dividend’ kwani watoto wao wanapata elimu bora, sisi hata hatujiandai na ‘demographic Bomb’ litakaloletwa na kundi kubwa la vijana wasio na elimu wala ujuzi.

Shiriki kurejesha Tanzania yenye kutoa fursa kwa kila raia bila kujali hali yake ya kipato.

Shirika kurejesha Tanzania yenye Usawa kwenye fursa na yenye demokrasia. Jiunge na CHADEMA tuendeleze mapambano.

Nawashukuru kwa kunisikiliza.

Zitto Kabwe, Mb

Naibu Katibu Mkuu CHADEMA

HIVI NDIVYO DIAMOND ALIVYOPERFORM KATIKA EVICTION PARTY YA BBA 7
Msanii Diamond alikuwa nchini Afrika Kusini Jumapili hii kwa ajili ya performance maalum wakati wa Eviction Party ya Big Brother Africa.Hivi ndivyo ilivyokuwa performance yake ya wimbo Mawazo

<object classid='clsid:d27cdb6e-ae6d-11cf-96b8-444553540000' codebase='http://macromedia.com/cabs/swflash.cab#version=9,0,0,246' id='dstvLrg' width='536' height='400'><param name='movie' value='http://core.dstv.com/video/flash/dstv_videoplayer.swf' /><param name='flashvars' value='base_url=http://ondemand.dstv.com/videofeeds/FreeVideoFeed.aspx?&id=198751' /><param name='quality' value='high' /><param name='allowscriptaccess' value='always' /><param name='allowfullscreen' value='true' /><embed src='http://core.dstv.com/video/flash/dstv_videoplayer.swf' allowfullscreen='true' flashvars='base_url=http://ondemand.dstv.com/videofeeds/FreeVideoFeed.aspx?&id=198751' width='536' height='400' type='application/x-shockwave-flash' allowscriptaccess='always'></embed></object>

NI HAWA PEKE YAO? TUFANYEJE NA WENGINE?
Nakumbuka nilipokuwa mdogo kuna ka wimbo tulipenda sana kukaimba. Kama sio kuimba basi ilikuwa ni kusema. Unashika vidole vya mkono(wa kulia au kushoto,haijalishi) na kuanza kusema, cha kwanza kinasema TWENDE cha pili kinauliza WAPI, cha tatu kinasema TUKAIBE, cha nne kinaitikia TUKIKAMATWA? Cha tano ambacho mara nyingi kilikuwa cha dole gumba kinasema MIE SIMO.

Nimekumbuka kale ka wimbo baada ya kutafakari kidogo kuhusu nchi yetu Tanzania na hususani matukio ya hivi karibuni ambayo yalisababisha muundo mpya wa Baraza la Mawaziri. Nimewaza kwa sauti zaidi niliposoma mahali kwamba baadhi ya  majalada ya Mawaziri unaowaona pichani yametua mezani kwa Dr.Hoseah pale TAKUKURU(Taasisi hii ningependa sana kujua mafanikio yake ikilinganishwa na gharama za uendeshaji wake)

Tafakari yangu imejikuta ikikwama katika swali moja; Je,hawa ninaowaona kwenye picha hapo juu ndio mawaziri au viongozi pekee wanaofanya “madudu” au kinyume cha yale wanayotakiwa kufanya au yale ambayo wanakuwa waliyasimamia majukwaani wakati wa kuomba ridhaa ya wananchi ya kuwaongoza?

Au hawa ni vile vidole vinne vya mwanzo na wengine waliobakia HAWAMO? Kama sio hao tu,basi TAKUKURU wanasubiri nini? Hivi inawezekana vipi katika Wizara moja Waziri afanye “ndivyo sivyo” na wakurugenzi,makatibu wakuu na wengine wawe salama tu? Hawakuona?Walisema nini?Any Whistle Blowers? Kama hawapo,hawahusiki kwa njia moja au nyingine? Tunapomuondoa Waziri,tatizo tumelitatua?

Utaona mashaka yangu hapo juu.Naamini kuna wengine.Wenyewe wanajiona wajanja. Wanakula kuku kwa mrija(nasema tu maana sijui hata ukinipa mrija na kuku nitamlaje)

Kinachoweza kuniondoa mashaka ni utendaji mpya. Imani ikishatoweka ni vigumu kuirudisha.Unajua hivyo na mimi naafiki.

Pichani Mawaziri walioondolewa ambao ni  pamoja na aliyekuwa wa Fedha, Mustafa Mkulo, Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), William Ngeleja (Nishati na Madini), Dk Cyril Chami (Viwanda na Biashara), Dk Hadji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii) na Omary Nundu (Uchukuzi).

SEAN KINGSTON AFUNGULIWA KESI NA BABA MWENYE NYUMBA!
Msanii Sean Kingston yupo matatani.Kwanini? Ni hivi, aliyekuwa mwenye nyumba wake wa huko Miami,Florida, amefungua kesi akidai kwamba msanii huyo amesababisha uharibifu mkubwa katika nyumba aliyokuwa akipanga kwa kiasi cha dola $25,000 kwa mwezi na pia amevunja mkataba wa upangaji.

Sean Kingston ambaye ni miongoni mwa wasanii kutoka US waliowahi kutua Tanzania anadaiwa kwamba yeye na mama yake walipanga nyumba hiyo tangu October mwaka jana kabla ya kuamua kuondoka tu ghafla mwaka huu kabla mkataba haujaisha. Mwenye nyumba anasema licha ya kuondoka ghafla, wapangaji wake hao wametia hasara ya $21,397 kutokana na kuharibu samani zilizopo katika nyumba hiyo.

Mwenye nyumba huyo pia anasema Sean Kingston na mama yake hawakulipa kodi ya pango kwa miezi miwili ya mwisho na hivyo anawataka walipe kiasi cha $73,816.85 ikiwa ni pango pamoja na riba.

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, mpaka hivi sasa kambi ya Sean Kingston haijasema chochote kuhusiana na kesi hiyo.

Bila shaka unaweza kujiuliza,inakuwaje msanii kama Sean Kingston, asiwe na nyumba yake mwenyewe kiasi kwamba awe mpangaji mpaka leo? Well…sijui lakini kumbuka hata Michael Jackson alifia kwenye nyumba ya kupanga!

MIAKA 54 ILIYOPITA MWALIMU JULIUS K.NYERERE ALIYASEMA HAYA…
Nimeipata hii katika e-mail moja inayosambaa na nimeipenda na kuona nikupe na wewe!

UZUSHI WA WIKIENDI(1)
Taratiiibuu mwisho wa wiki ndio umewadia. Wiki nyingine imekatika.Kufumba na kufumbua karibuni tunaanza kuutafuta mwezi kati.Nusu mwaka.Kama utani vile.

Kama ulikuwa umeweka malengo lukuki pale mwaka ulipoanza,basi nanii ishaanza kugonga nanihii. Unaona kama vile zilikuwa ndoto za alinacha mchana kweupe. Unapaniki nini sasa?Kwani ulivyokuwa unapanga mambo yako ulidhani wewe ni Mungu? Kubali matokeo,badilisha malengo. Nenda mbele kama vile morani anavyofukuzana na simba. Mkuku. Maisha ni kama kuendesha basikeli, huanguki mpaka uache kupiga chambi.

Mimi kama kawaida nipo. Leo naanzisha hiki kipengele cha Uzushi wa Wikiendi. Naangalia yale makubwa yaliyojiri katika wiki.Sijui nianzie wapi au nianze na lipi.Mambo kibao mezani kwangu.

Ooh nimekumbuka. Hivi si umesikia kwamba jamaa wa Ubungo kashinda mara ya pili? Ndio, mara ya pili kwa sababu mara ya kwanza wananchi walipoongea kuna mtu au watu hawakuamini. Haoo wakakimbilia kule kwa jamaa wanaovaa majoho. Bahati mbaya sana ni kwamba kule huwa sio bure. Kuna gharama zake. Zinaitwa gharama za uendeshaji. Lazima watu wanywe chai na biskuti ati.Ndio mpango mzima.

Basi jamaa wanaovaa majoho nao wakasema, Mama una haki ya kuleta malalamiko hapa kwetu.Ila siku nyingine, tuletee malalamiko yaliyo na tija. Hili halina kitu.Tupilia kule na gharama za uendeshaji kwako.Utalipa! Sheria bwana nishai.

Mara ghafla mji ukawa mdogo.Wafuasi wa “dogo” Mnyika wakaanza mambo yao.Mbwembwe,vibweka. Jamaa wa kijani, wakawa hawana jinsi bali kupisha tu wenyewe magwanda wapishe.Nasikia jamaa huwa ni matata sana.Ukiwaingilia raha zao itakula kwako. Na jamaa wanajua kushangilia sio kitoto. Watu na mtu wao bwana. Jama akabebwa kama vile enzi zile babu zetu walivyokuwa wakimbeba mkoloni.Babu zetu nao bwana…utakuta jamaa watano wenye misuli iliyoshiba kweli kweli wamekabeba kajamaa kamoja kazungu peke yake,tena wapo nacho msituni.Alah! Ningemtua kama ndoo..Fa mchezo nini?

Huku kwingine nako, kuna kipindi kipya cha luninga. Ni kupitia ile stesheni inayopendwa zaidi na watu wa rika la chini yaani vijana. Mdada anaitwa Mboni na kipindi chake kitaitwa Mboni Show. Mara watu ooh anadhani atakuwa Oprah wa Bongo…kwani jamani hata kama hatokuwa,kuna ubaya gani katika kujaribu? Hata huyo Oprah si alianza ndio kikaeleweka? Wasiwasi wangu ni mmoja tu…contents au yaliyomo. Haya mambo bwana yanataka sana uchunguzi wa kina.Yanataka upanue mawazo na mitizamo kweli kweli.Kwa maana nyingine usikome kujisomea na kujua kinachoendelea haswa. Sharti mtu akiangalia kipindi ajifunze kitu.Sio utolee macho luninga halafu ukimaliza kichwani kama banzoka.Noma.All in all twamtakia kheri Mboni. Chonga mpaka kieleweke.

Kule Jangwani napo kumechacha. Mwenyekiti kabwaga manyanga. Maji yamezidi unga.Ugali umekuwa uji. Yote hii ni kwa sababu chini ya uongozi wake,watoto wa Jangwani wakapokea kipigo cha mbwa mwitu kutoka kwa jamaa wa Msimbazi ambao wikiendi hii wanapanga kusababisha foleni kubwa.Wanashangilia ushindi.

Jamaa wa Jangwani wamesahau kabisa alichofanya huyu bwana.Kachukua sijui ubingwa.Kaondoa uteja wa Yanga kwa Simba.Watu hawataki kujua hiyo.Kwanini upokee kipigo kikali vile toka kwa Simba?Ndio soka la bongo lakini.Lipo zaidi midomoni kuliko uwanjani.Haya ngoja tuone kama kutakuwa na mpya baada ya Nchunga kubwaga manyanga.

Kwenye siasa nilichokiona kikubwa ni habari za yule Shibuda.Sijui jamaa anataka tu jina liwe kubwa zaidi au anaamini kabisa anachokiongelea. Angekuwa mbunge wangu yule,dah! Hebu kwanza niishie hapa hapa katika kumuongelea.

Mzee Mwandosya kaapishwa…hivi ni wiki hii au ya jana? Hana wizara maalumu!Hivi wewe unaweza kuamini kweli? Sasa sijui ofisi yake iko wapi tukamtembelee.Au ndio mambo ya “working from home”? Hii sijaipenda.Naomba niwe mkweli tu. Tunapoongelea kubana matumizi lazima tuwe siriasi wajameni.

Okay,ngoja niishie hapa kwa leo.Kama unapenda Uzushi wa Wikiendi uendelee,nitumie e-mail au niambie kupitia maoni. Uwe na wikiendi njema.

UNAWEZA KUIPA MANENO PICHA HII?
Kwa kimombo tunaweza kusema Can You Caption Me?

Pichani ni Mbunge wa Ubungo,John Mnyika(CHADEMA) akiwa na Hawa Ng’umbi mahakamani hapo jana wakati wa kusikiliza hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Hawa Ng’umbi kupinga matokeo ya Jimbo la Ubungo katika Uchaguzi Mkuu mwaka juzi ambapo Mnyika aliibuka mshindi.

Picha kwa hisani ya Bashir Nkoromo