New titles ASC Leiden
Dicionário de nomes em Oshikwanyama / Cecília Ndanyakukwa (Pandeinge).
<description><![CDATA[Município de Belas - Luanda-Sul, Angola : Mayamba Editora, 2016. 
. ASC Subject Headings: Angola. ; Kwanyama language. ; names. ; place names. ; proverbs (form) ; ]]></description>
<category>Angola.</category>
<category>Kwanyama language.</category>
<category>names.</category>
<category>place names.</category>
<category>proverbs (form)</category>
Mdhihiriko wa mkondo wa riwaya za kiforensiki : uchambuzi wa muktadha wa mahali katika riwaya pendwa teule / Neema Julius Luhwago.
<description><![CDATA[Dodoma, Tanzania : CHALUFAKITA, 2024 
. Jarida la CHALUFAKITA, volume 6, no. 1, p. 20-32. Abstract: "Makala hii inalenga kuudhihirisha mkondo wa riwaya za kiforensiki katika Riwaya ya Pendwa ya Kiswahili kupitia muktadha wa mahali kama unavyojipambanua. Utafiti wa makala hii ni wa kitaamuli. Data za makala hii zimekusanywa maktabani ambapo mbinu ya uchambuzi matini ilitumika. Nyaraka na riwaya teule zilisomwa na kuchambuliwa kwa mwongozo wa Nadharia ya Mwitikio wa Msomaji. Aidha, vipengele vya muktadha wa mahali vinavyoibua uchunguzi wa kiforensiki katika riwaya teule vimebainishwa. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kwamba mdhihiriko wa mkondo wa riwaya za kiforensiki katika riwaya pendwa ya Kiswahili ni mojawapo ya maendeleo ya riwaya pendwa ya Kiswahili hususani katika zama hizi za utandawazi na maendeleo ya sayansi na teknolojia." [Journal abstract]  Abstract: This article aims to demonstrate the emergence of the forensic novel trend in popular Swahili fiction, specifically analyzing how it manifests through the element of geographical setting. The study relies on a qualitative design. Data was collected via library research through textual analysis, where selected documents and novels were read and analyzed under the guidance of the reader-response theory.  ASC Subject Headings: East Africa. ; Swahili language. ; popular literature. ; autopsy. ; literary criticism. ;  https://www.ajol.info/index.php/jclfkt/article/view/297227 (free access)]]></description>
<category>East Africa.</category>
<category>Swahili language.</category>
<category>popular literature.</category>
<category>autopsy.</category>
<category>literary criticism.</category>
Utayari wa walimu tarajali kufundisha stadi za tafakuri tunduizi katika somo la Kiswahili : mfano teule wa ndaki ya elimu, chuo kikuu cha Rwanda / Laurien Tuyishimire and Patrice Ntawigira.
<description><![CDATA[Dodoma, Tanzania : CHALUFAKITA, 2024 
. Jarida la CHALUFAKITA, volume 6, no. 1, p. 1-19. Abstract: "Makala hii inakusudia kujibu maswali yafuatayo: Walimu tarajali wanaandaliwa namna gani kufundisha stadi za tafakuri tunduizi katika somo la Kiswahili? Walimu tarajali wana uelewa gani kuhusu stadi za tafakuri tunduizi na umuhimu wake kwa wanafunzi wa lugha ya Kiswahili? Walimu tarajali wana maoni gani kuhusu mikakati faafu ya kufundisha stadi za tafakuri tunduizi katika somo la Kiswahili? Ili kufanikisha lengo hili, data za kitaamuli zilikusanywa kwa kutumia mahojiano na uchambuzi wa matini. Data hizo zilichambuliwa kwa kuongozwa na Nadharia ya Tabia Iliyotambulika. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba walimu tarajali wanaandaliwa vema kufundisha stadi za tafakuri tunduizi katika somo la Kiswahili. Aidha, matokeo ya utafiti yameonesha kuwa walimu tarajali wana uwezo wa kufasili stadi za tafakuri tunduizi na kubainisha umuhimu wake kwa wanafunzi wa lugha, hususani ile ya Kiswahili. Vilevile, walimu tarajali wana utayari wa kufundisha stadi za tafakuri tunduizi katika somo la Kiswahili kupitia mikakati mbalimbali waliyoibainisha: mijadala, midahalo, na kazi za utatuzi wa tatizo. Pamoja na hayo, makala inapendekeza kuongezwa kwa mazoezi zaidi ya kuwazoeza kufundisha darasani ili yawasaidie kumahiri mikakati mbadala ya kufundisha stadi za tafakuri tunduizi." [Journal abstract]  Abstract: This article examines how student teachers are prepared to teach critical thinking skills within the Swahili language subject. Specifically, the study addresses three main questions: how student teachers are trained for this task, their understanding of critical thinking skills and their importance for Swahili language learners, and their opinions on the most effective strategies to teach these skills.  ASC Subject Headings: Rwanda. ; Swahili language. ; language instruction. ; cognition. ;  https://www.ajol.info/index.php/jclfkt/article/view/297226 (free access)]]></description>
<category>Rwanda.</category>
<category>Swahili language.</category>
<category>language instruction.</category>
<category>cognition.</category>
Matumizi ya msamiati katika jamiilugha ya wafanyabiashara wa soko la karume katika jiji la Dar Es Salaam / Sauda Uba Juma.
<description><![CDATA[Dodoma, Tanzania : CHALUFAKITA, 2023 
. Jarida la CHALUFAKITA, volume 5, no. 1, p. 80-92. Abstract: Makala hii inalenga kubainisha msamiati maalumu wa Kiswahili unaoibuliwa na wafanyabiashara wanaouza viatu vya mtumba katika soko la Karume jijini Dar es Salaam. Aidha, inalenga kuchunguza jinsi wafanyabiashara hao wanavyoutumia msamiati huo katika mchakato mzima wa kuendesha biashara zao katika miktadha mbalimbali. Utafiti huu, ni matokeo ya data za uwandani za usaili na ushuhudiaji. Data zingine zilipatikana maktabani kupitia usomaji wa nyaraka zinazoakisi mada hii kama vile: vitabu, tasnifu pamoja na majarida mbalimbali. Mbinu zote hizo kwa pamoja zimemsaidia mtafiti kupata data faafu zinazotosha kujibu lengo la makala hii. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi wa Kimaeneo ya Fishman (1972) na data zimechanganuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Kwa ujumla, matokeo ya uchunguzi yameweka wazi msamiati fiche wa Kiswahili unaotumiwa na wafanyabiashara hao. Hivyo, tunapendekeza msamiati huo upitiwe na vyombo vilivyopewa dhamana ya kuunda istilahi, ili kuona namna bora ya kuweza kuusanifisha. [Journal abstract]  Abstract: This article identifies the specialized Swahili jargon used by second-hand shoe traders at the Karume Market in Dar es Salaam and examines how they apply it across various business contexts.  ASC Subject Headings: Tanzania. ; traders. ; Swahili language. ; sociolects. ;  https://www.ajol.info/index.php/jclfkt/issue/view/25850 (free access)]]></description>
<category>Tanzania.</category>
<category>traders.</category>
<category>Swahili language.</category>
<category>sociolects.</category>
Changamoto zinazowakabili walimu wa kiswahili katika utekelezaji wa mtaala wa Umilisi : mfano wa shule teule za sekondari wilayani nyagatare, Rwanda / Martin Hubert Ikuramutse.
<description><![CDATA[Dodoma, Tanzania : CHALUFAKITA, 2023 
. Jarida la CHALUFAKITA, volume 5, no. 1, p. 27-41. Abstract: Makala hii ina malengo mahsusi mawili: kubainisha changamoto zinazowakabili walimu wa Kiswahili katika utekelezaji wa Mtaala wa Umilisi na kubainisha mikakati na mapendekezo ya kukabiliana na changamoto hizo. Sampuli ya utafiti iliundwa na wanafunzi 30, walimu wa Kiswahili 3 na wakuu wa masomo 3. Hii ni kwa kuwa kila shule ina mwalimu na mkuu wa masomo mmoja tu. Eneo la utafiti lilikuwa Wilaya ya Nyagatare. Data zilipatikana kupitia ushuhudiaji, mahojiano, na udurusu wa nyaraka kutoka kwenye majarida, mtandao, tasnifu na makala mbalimbali. Data zilichanganuliwa kwa kutumia Nadharia ya Utekelezaji wa Mtaala iliyoasisiwa na Gross mwaka 1971. Kisha, ziliwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Changamoto zilizobainika ni uhaba wa vifaa vya ufundishaji, uwezo mdogo wa lugha ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi, uhaba wa mafunzo walimu, mtazamo hasi wa walimu kuhusu matumizi ya TEHAMA, ukosefu wa ushirikiano kati ya walimu na wazazi, na mtazamo hasi wa walimu kuhusu Mtaala wa Umilisi. Makala hii inapendekeza uongezaji wa rasilimali za kufundishia, ushirikiano wa wakuzaji wa mtaala na wadau wengine, na utoaji wa mafunzo ya walimu kuhusu mbinu bora za ufundishaji wa Kiswahili katika mazingira ya Mtaala wa Umilisi. [Journal abstract]  Abstract: This article identifies the challenges faced by Swahili teachers in implementing the Competency-Based Curriculum (CBC) in Rwanda and outlines strategies to overcome them. Conducted in the Nyagatare District, the study used a sample size consisting of 30 students, 3 Swahili teachers, and 3 heads of departments.Data was collected through observations, interviews, and document reviews, and was subsequently analyzed using Gross's (1971) Curriculum Implementation Theory.  ASC Subject Headings: Rwanda. ; curriculum. ; Swahili language. ; language instruction. ;  https://www.ajol.info/index.php/jclfkt/article/view/295878 (free access)]]></description>
<category>Rwanda.</category>
<category>curriculum.</category>
<category>Swahili language.</category>
<category>language instruction.</category>
Viashiria vya ufungwa wa kisaikolojia kwa wahusika katika riwaya ya kiswahili : mifano kutoka 'vuta n’kuvute na kufikirika' / Zuhura Ismail Said and Zuhura A. Badru.
<description><![CDATA[Dodoma, Tanzania : CHALUFAKITA, 2023 
. Jarida la CHALUFAKITA, volume 5, no. 1, p. 12-26. Abstract: Makala hii imelenga kufafanua ufungwa wa kisaikolojia kwa kubainisha viashiria vyake katika riwaya teule. Nadharia iliyoongoza ukusanyaji, uchambuzi na uwasilishaji wa data za makala hii ni Nadharia ya Saikolojiachanganuzi. Aidha, usanifu uliotumika katika makala hii ni uchunguzi kifani. Makala hii ni sehemu ya utafiti uliofanyika kwa mahitaji ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Hivyo, data zake zilipatikana maktabani kupitia utafiti uliofanywa 2023. Data za maktabani zilipatikana kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini, hususani kusoma na kuchambua riwaya teule. Matokeo yanaonesha kwamba viashiria vya ufungwa wa kisaikolojia kwa wahusika katika riwaya teule vinadhihirika kupitia vilio, manung’uniko na uteti, hali ya unyonge na kukata tamaa na kufanya matendo yasiyo ya kawaida kwa wahusika wa kazi hizo. [Journal abstract]  Abstract: This article aims to explain psychological imprisonment by identifying its indicators in selected Swahili novels. The data was collected in 2023 through library research and analyzed using textual analysis, focusing on reading and examining the selected novels (Vuta N’kuvute by Adam Shafi and Kufikirika by Shaaban Robert).  ASC Subject Headings: Tanzania. ; Swahili language. ; novels. ; literary criticism. ;  https://www.ajol.info/index.php/jclfkt/article/view/295877 (free access)]]></description>
<category>Tanzania.</category>
<category>Swahili language.</category>
<category>novels.</category>
<category>literary criticism.</category>
Usawiri wa mawazo ya kidhanaishi katika fasihi simulizi ya kiswahili : uchunguzi kifani wa nyimbo teule za bongofleva / Christopher B. Lucas and Mashaka H.K. Ng’waje.
<description><![CDATA[Dodoma, Tanzania : CHALUFAKITA, 2023 
. Jarida la CHALUFAKITA, volume 5, no. 1, p. 1-11. Abstract: Makala hii inahusu usawiri wa mawazo ya kidhanaishi katika fasihi simulizi kwa kumakinikia nyimbo za Bongofleva. Uchunguzi huu ulichochewa na pengo la kimaarifa linaloibua fikra tunduizi zinazoshuku kuwapo kwa mawazo ya kidhanaishi katika fasihi simulizi ya Kiswahili. Data za makala hii zilikusanywa kutoka katika nyimbo tatu za Bongofleva kwa kutumia njia ya uchanganuzi matini. Data hizo zilichambuliwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli huku tukiongozwa na Nadharia ya Udhanaishi iliyoasisiwa na Soren Kierkegaard. Nadharia hii imetuongoza kubaini kuwa fasihi simulizi kama ilivyo fasihi andishi, husawiri mawazo ya kidhanaishi. Matokeo haya yalifikiwa kutokana na kujitokeza kwa mawazo mbalimbali ya kidhanaishi katika nyimbo teule za Bongofleva. Mawazo hayo ni kama vile, maisha ya ndoa hayana furaha bali ni karaha tupu, Mungu hayupo, kila mwanadamu atawajibika kwa matendo yake mwenyewe na maisha hayashibishi wala kuridhisha. Kutokana na matokeo hayo, makala hii imehitimisha kuwa karaha za maisha ndizo huwafanya fanani kusawiri mawazo ya kidhanaishi katika kazi zao. Kwa msingi huo, mawazo ya kidhanaishi hayaishii tu katika fasihi andishi, bali hupenya pia hata katika fasihi simulizi. Vilevile, makala hii imependekeza kuwa tafiti zisifungwe na kuchunguza udhanaishi katika kazi zilizoandikwa na Euphrase Kezilahabi tu, bali ziende mbali zaidi kwa kuchunguza kazi za waandishi wengine. Hali hii itapanua mawanda na nadharia hii katika fasihi ya Kiswahili. [Journal abstract]  Abstract: This article examines how existentialist ideas are portrayed in oral literature, specifically focusing on Bongo Flava songs. Driven by a gap in research regarding existentialism in Swahili oral literature, the study analyzes text from three selected Bongo Flava songs using a qualitative approach guided by Søren Kierkegaard’s Existentialist Theory.  ASC Subject Headings: Tanzania. ; Swahili language. ; songs. ; literary criticism. ;  https://www.ajol.info/index.php/jclfkt/article/view/295876 (free access)]]></description>
<category>Tanzania.</category>
<category>Swahili language.</category>
<category>songs.</category>
<category>literary criticism.</category>
Kategoria za utumwa katika fasihi ya Kiswahil : uchunguzi wa kazi teule / Ernesta S. Mosha na Grace H. Minja.
<description><![CDATA[Dar es Salaam : Institute of Kiswahili Studies, University of Dar es Salaam, 2025. 
. Kioo cha Lugha,, volume 23, no. 2, p. 181-205. Abstract: "Utumwa ni mfumo ambao hulazimisha watu kufanya kazi au jambo fulani bila malipo au ridhaa. Kuna aina kuu mbili za utumwa, yaani utumwa wa kijadi na utumwa wa kisasa3. Utumwa wa kijadi unahusu watu kuuzwa kama bidhaa na kwenda kutumikishwa sehemu kama vile kwenye mashamba makubwa, migodini na majumbani. Ni utumwa ulioanza zamani sana na ulikuwapo katika jamii kwa karne nyingi. Madhara ya utumwa wa kijadi bado hayajafutika katika historia za jamii husika. Kwa upande mwingine, utumwa wa kisasa ni ule unaojitokeza kwa namna nyingi kama vile: utumwa wa kifikra, kimapenzi, madeni, na kutumikisha watoto wadogo. Aina hii ya utumwa, licha ya kuonekana kuwa umeshika kasi sana katika zama hizi za utandawazi, kwa hakika, baadhi ya aina zake zimekuwa katika jamii kwa muda mrefu. Makala hii imejadili namna fasihi ya Kiswahili inavyosawiri utumwa wa kijadi na aina anuwai za utumwa wa kisasa. Kwa kutumia Nadharia ya Mwingilianomatini, riwaya nne za fasihi ya Kiswahili - Uhuru wa Watumwa (1934), Kasri ya Mwinyi Fuad (1987), Kwaheri Iselamagazi (1992) na Miradi Bubu ya Wazalendo (1995) zimechunguzwa ili kuweka bayana suala hili. Imebainika kuwa utumwa wa kisasa una madhara ambayo hayajulikani mapema ikilinganishwa na utumwa wa kijadi kwa sababu madhara hayo hayaonekani waziwazi kwa kuwa yapo ndani ya utu wa mhusika. Pia, utumwa wa kisasa, kama vile utumwa wa kifikra na utumwa wa madeni unachangia katika utokeaji na/au uimarishaji wa utumwa wa kijadi." [Journal abstract]  Abstract: This article examines the representation of slavery in Swahili literature, distinguishing between traditional slavery and modern forms of slavery. Traditional slavery refers to the historical practice of treating people as property and forcing them to work on plantations, in mines, or in households. Although this form of slavery belongs largely to the past, its effects remain evident in the histories of affected societies. Modern slavery, by contrast, takes various forms, including mental or ideological enslavement, romantic or emotional dependence, debt bondage, and child labour. While these forms appear especially prevalent in the era of globalization, some have existed in society for a long time. Using Intertextuality Theory, the study analyzes four Swahili novels: Uhuru wa Watumwa (1934), Kasri ya Mwinyi Fuad (1987), Kwaheri Iselamagazi (1992), and Miradi Bubu ya Wazalendo (1995). The analysis shows that modern slavery can be more difficult to recognize than traditional slavery because its harmful effects are often hidden within an individual's identity and lived experience rather than being openly visible. The study further argues that modern forms of slavery, particularly mental enslavement and debt bondage, can contribute to the emergence and reinforcement of traditional forms of slavery.  ASC Subject Headings: East Africa. ; novels. ; slavery. ; Swahili language. ; literary criticism. ;  https://journals.udsm.ac.tz/index.php/kcl/article/view/9608 (free access)]]></description>
<category>East Africa.</category>
<category>novels.</category>
<category>slavery.</category>
<category>Swahili language.</category>
<category>literary criticism.</category>
Biashara ya utumwa Mashariki mwa Congo na athari zake katika lugha ya Kiswahili / Kalunga Mwela-UBI Marcel na Kilongozi SI Umba Jean.
. Kioo cha Lugha,, volume 23, no. 2, p. 150-180. Abstract: "Kama ilivyo kwa viumbe vilivyo hai, lugha inapitia kwenye nyakati tatu muhimu: kuzaliwa, kukua na kufa. Kila wakati unatokana na sababu zake ambazo, mara nyingi, hazihusiki moja kwa moja na lugha yenyewe. Baadhi ya sababu hizi zinaambatana na mazingira ya eneo ambamo lugha inatumiwa: historia, uchumi, teknolojia, saikolojia, mawasiliano na lugha za maeneo mapya. Kuwapo kwa biashara ya watumwa kati ya Afrika Mashariki na Afrika ya Kati ni mojawapo ya njia zilizochangia kuingiza Kiswahili kwenye mikoa ya Mashariki mwa Congo. Wakaaji wa mikoa hii huzungumza kwa kiwango kikubwa sana lugha za Kibantu. Hali hii inaeleza urahisi wa maingiliano ya Kiswahili, kwa upande mmoja, na lugha za maeneno haya, kwa upande mwigine. Lengo la makala hii siyo kuelezea historia ya biashara ya watumwa katika maeneo yaliyotajwa hapo juu, bali ni kuonesha ni kwa namna gani lugha ya Kiswahili iliathirika kutokana na kuingizwa kwake nchini Congo. Kwa hiyo, makala inatilia mkazo wa pekee katika kutoa baadhi ya athari katika fonolojia, mofolojia, leksikolojia na semantiki ikilinganisha lahaja mbili hizi za Kiswahili: Kiswahili cha Afrika Mashariki na kile cha nchi ya Congo." [Journal abstract]  Abstract: This text focuses on the expansion of Swahili into eastern Congo—initially driven by the East and Central African slave trade—and notes how its integration was eased by the region's existing Bantu-speaking population. Rather than detailing the history of the slave trade, the text highlights how Swahili was affected by its introduction to Congo, specifically examining the phonological, morphological, lexical, and semantic differences between East African Swahili and Congolese Swahili.  ASC Subject Headings: East Africa. ; Swahili language. ; dialects. ;  https://journals.udsm.ac.tz/index.php/kcl/article/view/9609 (free access)]]></description>
<category>East Africa.</category>
<category>Swahili language.</category>
<category>dialects.</category>
Utumwa na maisha baada ya utumwa katika Jamii za Afrika Mashariki : historia, lugha na fasihi ya Kiswahili / Salvatory S. Nyanto na Angelus Mnenuka.
. Kioo cha Lugha,, volume 23, no. 2, p. 123-133. Abstract: This introductory section provides background on slavery and post-slavery in various societies found in the East African region.  ASC Subject Headings: East Africa. ; slavery. ; history. ; Swahili language. ;  https://journals.udsm.ac.tz/index.php/kcl/article/view/9723 (free access)]]></description>
<category>East Africa.</category>
<category>slavery.</category>
<category>history.</category>
<category>Swahili language.</category>
Manyezi ya utumwa katika makutano ya utumwa na ukoloni na athari yake katika usemi wa kitamaduni na mtazamo wa Jamii za Afrika Mashariki / Ali H. Chembea.
. Kioo cha Lugha,, volume 23, no. 2, p. 319-330. Abstract: "Utumwa ni suala linalozua si tu manyezi katika fasihi ya Kiswahili bali pia linaakisi utata wa kihistoria na kijamii katika Ukanda wa Afrika Mashariki. Fasihi ya Kiswahili imekuwa chemchemi yenye nguvu kueleza sauti za waliotengwa, kutambua hali halisi ya maisha ya utumwa, upinzani na ustahimilivu. Uchunguzi huu umeshughulikia makutano ya ukoloni na utumwa, ukionesha jinsi nguvu hizi zinavyoingiliana kuathiri usemi wa kitamaduni na mitazamo ya jamii. Kupitia diwani ya Sauti ya Dhiki iliyoandikwa na Abdilatif Abdalla na riwaya ya Kasri ya Mwinyi Fuad iliyoandikwa na Adam Shafi ndani ya mifumo mipana ya kihistoria, waandishi wameonesha mateso ya kihisiamoyo na ya kimwili ya watumwa, hasa katika kuangazia mapambano yao ya kupata uhuru na utu. Makala hii inachanganua umuhimu wa kuelewa utumwa si tu kama ukweli wa kihistoria bali kama masimulizi yenye nguvu ambayo yanaendelea kuvuma katika matini za fasihi ya Kiswahili. Hatimaye, uchunguzi huu umesawiri ufahamu wa kina wa athari za utumwa, ukiangazia jukumu lake katika kujenga utambulisho wa kitamaduni na kukuza diskozi za kijamii katika mapambano yanayoendelea ya haki na utu." [Journal abstract]  Abstract: Swahili literature serves as a powerful medium for giving voice to the marginalized, exposing the physical and emotional trauma of slavery, and exploring the ongoing struggle for freedom and human dignity. Rather than treating slavery merely as a past event, Swahili authors use it as a resonant narrative to confront the complex historical, social, and colonial intersections that shaped East African society. Analyzing Abdilatif Abdalla's poetry collection 'Sauti ya Dhiki' and Adam Shafi's novel 'Kasri ya Mwinyi Fuad', this article demonstrates how these literary works depict both the suffering and the resilience of enslaved people. Ultimately, the study highlights how narratives of slavery continue to influence cultural identity, foster social discourse, and drive the ongoing struggle for justice and human dignity in East Africa.  ASC Subject Headings: East Africa. ; literature. ; Swahili language. ; enslaved persons. ; literary criticism. ;  https://journals.udsm.ac.tz/index.php/kcl/article/view/9615 (free access)]]></description>
<category>East Africa.</category>
<category>literature.</category>
<category>Swahili language.</category>
<category>enslaved persons.</category>
<category>literary criticism.</category>
Minyiri ya utumwa : lugha na mtanziko wa fikra za kikoloni miongoni mwa Waafrika / Aldin Kai. Mutembei.
. Kioo cha Lugha,, volume 23, no. 2, p. 271-276. Abstract: "Maana ya utumwa imekuwa sehemu mojawapo ya mada katika mijadala ya wanazuoni hasa baada ya mwaka 1926. Mpaka mwaka 2012, bado kulikuwa na mjadala wa kisheria kuhusu maana ya utumwa. Mijadala hii haikuangalia sana suala la lugha kama nyenzo yenye kuingiza dhana ya kipekee katika maana ya utumwa. Hata hivyo, ni wazi kuwa wakati wa utumwa wa Waarabu, lugha ilitumika kuufanikisha utumwa. Lugha iliubeba utumwa. Wakati wa ukoloni mkongwe, lugha za kikoloni zilijenga matabaka ya kitumwa. Minyiri ya utumwa-lugha ikajiviringa na kuwavunganiza watumwa kifikra na kuwafanya wajikane. Wakati huu wa ukoloni mamboleo, utumwa-lugha umeifanya fikra ya aliyetawaliwa kushikwa na minyiri ya kikoloni kiasi cha kujikuta katika mtanziko: alikotoka hakujui, na kama kuna aendako, hakufahamu. Makala hii ikiongozwa na mawazo ya Frantz Fanon kuhusu lugha (2008), imetumia dhana ya utumwa-lugha kujadili jinsi lugha za watawala wa kikoloni barani Afrika zinavyotokeza utumwa wa kifikra, ambao hatimaye unaharibu misingi mikuu ya kuwapo kwa Mwafrika. Kupitia utumwa-lugha, Waafrika wameachwa katika mtanziko mkubwa wenye mivutano ya ndani inayojibadilisha kuwa minyiri isiyoweza kukatwa na kung‘olewa bila ya kuwa na mapinduzi ya kifikra." [Journal abstract]  Abstract: Language serves as a tool for mental enslavement that undermines the core existence of African people, extending far beyond the historical legal definitions debated by scholars between 1926 and 2012. Throughout the eras of Arab slavery, classical colonialism, and modern neocolonialism, dominant colonial languages have systematically built social classes and trapped the minds of the colonized. Guided by Frantz Fanon's framework on language (2008), this article utilizes the concept of linguistic slavery (utumwa-lugha) to explore how colonial languages cause deep psychological alienation. This leaves Africans in a profound internal crisis—disconnected from their past and uncertain of their future. The study concludes that these invisible linguistic shackles cannot be broken without a total intellectual revolution.  ASC Subject Headings: Africa. ; languages. ; colonialism. ;  https://journals.udsm.ac.tz/index.php/kcl/article/view/9614 (free access)]]></description>
<category>Africa.</category>
<category>languages.</category>
<category>colonialism.</category>