Tanzania News - Tanzania Latest News, International News, Tanzania Local News, All Tanzania News, News for Tanzania, News from Tanzania, Tanzania, News!

Anayedaiwa kumuua Barlow akamatwa
Frederick Katulanda, Mwanza
MTU mmoja anayeshukiwa kuwa ndiye aliyehusika kumpiga risasi na kumuua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (53), amekamatwa na polisi mkoani Mwanza.

Kamanda Barlow aliuawa kwa kupigwa risasi shingoni usiku wa manane wakati akimsindikiza mwanamke mmoja baada ya kuhudhuria kikao cha harusi ya ndugu yake.

Mtuhumiwa huyo anaaminika kuwa ndiye aliyehusika na kumpiga risasi, na inadaiwa kuwa ana rekodi ya kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu.

Ilielezwa kuwa mtuhumiwa huyo kabla ya kuhusika na mauaji hayo, alitoka jela miezi minne iliyopita.
Habari za uhakika kutoka ndani ya jeshi hilo pamoja na timu ya makachero wanaohusika na uchunguzi wa mauaji hayo chini ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, zimeeleza kwamba, kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumetegua kitendawili cha chanzo cha mauaji hayo na kubainisha kuwa hayahusiani na mapenzi.

“Jana (juzi) ilikuwa ni siku muhimu kwa Jeshi la Polisi, mtu muhimu sana katika sakata la mauaji hayo alikamatwa, huyu kwa mujibu wa rekodi zetu anaonekana kuhusika na matukio kadhaa ya ujambazi na kabla ya ya mauaji ya kamanda wetu alikuwa jela,” kilieleza chanzo chetu.

Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo,  kunafanya waliokamatwa hadi sasa kufikia sita akiwamo Mwalimu Dorothy Moses.

Imeelezwa kwamba kupatikana kwa mtuhumiwa huyo, maelezo ya awali ambayo yalitolewa na Mwalimu Dorothy Moses pia yamebadilika kutokana na kuonekana ni mmoja wa watu wa karibu na mtuhumiwa huyo na kwamba zipo dalili za kuhusika katika njama hizo za mauaji.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Lili Matola alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, lakini hakutaka kuingia ndani kwa madai ya kwamba hiyo ilikuwa ni kazi ya DCI Manumba anayehusika na upelelezi huo.

“Naomba muwe na subira, mambo ni mazuri, kwani hatua za upelelezi wa mauaji ya Kamanda Barlow umefikia hatua nzuri, hayo mnayosema baadhi ni sahihi, lakini mengine nami nayasikia, ila tu la muhimu tuvute subira kwani ukweli wote utatangazwa,”alieleza.

Kutokana na uchunguzi huo kuingia katika hatua muhimu, ilielezwa kwamba DCI Manumba aliwasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Said Mwema ambaye aliwasili jana jijini Mwanza.

Baadaye Mwema  aliiwasilisha ripoti ya kukamatwa kwa mtuhumiwa katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Mkoa wa Mwanza chini ya Mkuu wa Mkoa Mhandisi Evarist Ndikilo.

Akitoa taarifa ya mauaji kwa waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba alisema watu 10 wanashikiliwa kwa mauaji hayo huku akitaja sababu za mauaji hayo kuwa ni kisasi cha mapenzi na ujambazi.

Manumba ambaye aliambatana na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Said Mwema alisema baada ya kupatikana simu ya Mwalimu Dorothy Moses aliyekuwa na marehemu kamanda huyo usiku wa tukio, walifanikiwa kukamatwa watuhumiwa watano jijini Dar es Salaam ambao wameonekana kuwa na rekodi ya kuhusika na matukio kadhaa ya ujambazi Mwanza na maeneo mengine nchini.

“Watu hawa ni majambazi, na kabla ya kumuua kamanda Mwanza inaonekana walihusika na matukio kadhaa ya ujambazi, na hata baada ya kukimbilia Dar es Salaam nako walihusika na matukio kadhaa na kufanikiwa kukamatwa ambapo wamekiri kuhusika na kutuwezesha kukamata silaha aina ya Shotgun pamoja na silaha nyingine aina ya Pumpaction,” alieleza DCI Manumba.

Kutokana na rekodi ya ujambazi na mmojawao kubainika kuwa alitoka jela miezi minne kabla ya tukio hilo, Jeshi la Polisi limedai kuwa sababu ya mauaji inaweza kuwa inatokana na ujambazi.

DCI Manumba alisema katika idadi hiyo ya watuhumiwa 10 bado jeshi lake linaendelea kuwasaka watu wengine wawili ambao wametajwa kuhusika na tukio hilo.

Uchaguzi wazidi kuipasua UVCCM
Mwandishi Wetu, Dodoma
SASA ni dhahiri kwamba matokeo ya uchaguzi wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), yameigawa jumuiya hiyo na huenda ikajikuta kwenye mgogoro mkubwa wa kiuongozi ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa.

Hali hiyo inatazamwa na baadhi ya wachunguzi wa mambo kwamba ni kutimia kwa utabiri wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete ambao aliutoa wakati akifungua mkutano huo kwamba lazima viongozi watakaochaguliwa wachukue hatua za kuondoa nyufa zitakazotokana na uchaguzi huo.

Kadhalika, Rais Kikwete aliwaambia UVCCM kwamba watajuta ikiwa watachagua viongozi wasio na uwezo kutokana na kushawishiwa na rushwa, kauli ambayo hata hivyo, vijana hao waliipuuza kwani uchaguzi huo ulidaiwa kugubikwa na vitendo hivyo hali iliyozua malalamiko kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa mkutano.

Wasiwasi wa kupasuka kwa UVCCM unatokana na wanaodaiwa kuwa wanachama wa jumuiya hiyo 379 wengi wakiwa wajumbe wa mkutano mkuu, kusaini tamko la kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi wa nafasi ya mwenyekiti, Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamisi na Makamu wake Mboni Mhita.

Kadhalika, hofu ya kukua kwa ufa huo, inatokana na ukimya wa aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Paul Makonda juu ya nafasi ya kuteuliwa kwake na Sadifa kuwa mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM.
Tofauti na mgombea mwenzake, Rashid Simai Msaraka aliyekubali uteuzi uliofanywa na Sadifa kumpa ujumbe wa baraza, Makonda hadi sasa hajaukubali wala kuukataa, ukimya unaotafsiriwa kuwa unaweza kuwa na ajenda kubwa ndani yake.

Hata hivyo, Makonda alipozungumza na Mwananchi jana alisema atatoa uamuzi wake baadaye pale atakapozungumza na vyombo vya habari kuhusu yaliyojiri katika uchaguzi wa UVCCM.

“Kwa sasa siwezi kusema nimekubali uteuzi huu au hapana, ninafanya hivi kwa sababu kama ulinisikia jana (juzi) nilisema uongozi tuliouchagua ni aina ya jumuiya tunayoitaka, sasa ni aina gani hiyo, nitazungumza na baada ya hapo nitatoa sababu za kukubali au kukataa uteuzi wa Sadifa,”alisema Makonda na kuongeza:

“Leo hii nikisema nakubali uteuzi huo, basi wapo watakaosema nimehongwa au nimerubuniwa, lakini pia nikisema naukataa wapo watakaosema nina uchungu wa kukosa uongozi, sasa subiri tu siku nikisema nakubali au nakataa nitatoa sababu”.

Kiini cha mvutano
Mvutano kuhusu ushindi wa viongozi hao wakuu wa UVCCM unatokana na kuwapo kwa madai kwamba uchaguzi mzima uligubikwa na vitendo vya rushwa kwa wajumbe, hivyo kuufanya kutokuwa huru na haki.
Mapema juzi, muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa, kundi la vijana kutoka mikoa mbalimbali walikutana na waandishi wa habari, na kulalamika kwamba rushwa ilitawala na kuwatuhumu viongozi wa juu wa UVCCM kwa kuonyesha upendeleo wa dhahiri kwa baadhi ya wagombea.

Vijana hao walisema taswira ya uchaguzi huo inadhihirisha kwamba ndani ya CCM hivi sasa mtu hawezi kupata uongozi ikiwa hatoi fedha, hali ambayo ni hatari kwani imeingia katika kundi la vijana.
Baadhi ya wagombea walioshindwa uchaguzi wakitoa shukrani kwa wajumbe walikubali kushindwa kwao isipokuwa Makonda ambaye alisema: “Heri kushindwa kwa heshima, kuliko kushinda kwa fedheha.”

Gazeti hili jana lilipomtaka Makonda atoe ufafanuzi wa kauli yake aliyoitoa juzi alisema: “Unawezaje kujivuna kwamba wewe ni mshindi wakati dhamiri yako ikijua kwamba ulitumia hila, fedha na ulaghai, huwezi kuwa na confidence (kujiamini) hata kidogo, sasa mtu asiyejiamini hiyo ni fedheha.”

Kwa upande mwingine, kundi la vijana wanaoongoza harakati za kutaka matokeo hayo yatenguliwe, jana liliwasilisha Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, baadhi ya vielelezo kuhusu kuwapo kwa vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo.

Taarifa zinasema  kundi hilo linaanda barua na kiambatanisho cha majina na saini za wanachama wa UVCCM 379 ambao mpaka sasa wamesaini tamko la kupinga matokeo ya uchaguzi huo kupeleka kwa uongozi wa CCM.
Mmoja wa maofisa wa CCM makao makuu mjini Dodoma ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe aliliambia gazeti hili kuwa: “Ni kweli wale vijana wameleta sehemu ya ushahidi wao na tumeupokea, ila tumewaelekeza kwamba lazima waandike barua ya malalamiko na iwe imefika sehemu husika katika muda wa siku 14 tangu kutangazwa kwa matokeo”.

Hatua ya vijana hao ni kama wanakubaliana na ushauri waliopewa na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela na aliyekuwa mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM lililopita, Hussein Bashe kwamba wafuate taratibu za kawaida za malalamiko ikiwa hawakuridhika na matokeo.

Juzi kwa nyakati tofauti, Shigela na Bashe walituhumiwa kwamba walijihusisha na vitendo vya rushwa ikiwa ni pamoja na kuwashawishi wajumbe wa mkutano kuwapigia kura baadhi ya wagombea, lakini viongozi hao walikanusha tuhuma hizo.

Gazeti hili jana liliwatafuta Sadifa na Mboni ili kuzungumzia malalamiko yanayotolewa kuhusu ushindi wao, lakini jitihada hizo hazikufanikiwa kwani walikuwa kwenye kikao cha kwanza cha Baraza Kuu la jumuiya hiyo.

Madiwani wa Chadema watwangana Moshi
Daniel Mjema, Moshi na Suzy Butondo Shinyanga
MADIWANI wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika Manispaa ya Moshi, Kilimanjaro juzi walitwangana makonde huku kiini kikitajwa kuwa ni gari la Mstahiki Meya.

Tukio hilo linadaiwa kutokea juzi katika moja ya kumbi za mikutano ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakati madiwani hao wakiwa katika kikao cha ndani cha maandalizi ya mkutano wa baraza la madiwani.
Hata hivyo, licha ya taarifa za tukio hilo kuzagaa haraka, wahusika wameifanya siri ili kulinda heshima ya chama hicho.

Inadaiwa kuwa kisa cha kupigana ni ubishi juu ya nani anastahili kupanda gari hilo la Meya na baada ya kurushiana maneno, madiwani hao walivaana na kuanza kupigana kabla ya kuamuliwa na wenzao.
Habari zinadai kuwa madiwani watatu wamekuwa wakilitumia gari la Meya kila wanapolihitaji bila kikwazo jambo ambalo limekuwa likiwakera baadhi yao.

Mwenyekiti wa Madiwani wa CCM katika Baraza hilo, Michael Mwita amekiri kuarifiwa juu ya tukio hilo lakini hakulishuhudia akisema alikuwa katika ukumbi mwingine.
Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael hakupatikana kuzungumzia tukio hilo kwani tangu juzi, simu yake imekuwa ikiita bila kupokewa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Bernadette Kinabo alisema amesikia kutokea kwa tukio hilo.

Alisema tukio hilo limemsikitisha na kuwataka madiwani kuhimili jambo hata kama ni kutukanwa... “Nimearifiwa juu ya jambo hilo japo si kwa undani sana. Ila kwa kweli madiwani wanapaswa kujiheshimu ili na wengine wajifunze kutoka kwao. Haipendezi madiwani kutumia lugha ya kuudhi zaidi yao na anayetolewa lugha hiyo naye lazima azuie jazba.”

Mwenyekiti Chadema achomwa mkuki

Mwenyekiti wa Chadema, Tawi la Mwawaza, Shinyanga, Bundala Katunge amechomwa mkuki baada ya kuvamiwa na
kushambuliwa na kundi la watu zaidi ya 30.
Tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Mwawaza saa tano usiku akiwa amelala nyumbani kwake.
Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa Katunge alijeruhiwa baada ya kutoka nje ya nyumba yake mara baada ya kusikia bendera ya Chadema ikishushwa kwenye mlingoti.

Ilidaiwa kuwa alijaribu kuwazuia lakini walimzidi nguvu na kuanza kumshambulia. Aliwaponyoka na kuanza kukimbia ndipo mmojawao alipomrushia mkuki na kumchoma sehemu za mbavu upande wa kushoto. Baada ya tukio hilo  kundi hilo lilitoweka.

Katibu wa Chadema Wilaya ya Shinyanga, Nyangaki Shilungushela alisema Katunge alikimbilia kwa majirani ambao walimpeleka katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga ambako alifanyiwa upasuaji na kulazwa akisema hali yake ni mbaya.

Mganga Mfawidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Frederick Mlekwa alikiri kuwapo kwa mgonjwa huyo na kusema anaendelea kupatiwa matibabu.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala alisema hana taarifa ya tukio hilo.
Hata hivyo, wananchi wa eneo hilo walisema jana kwamba tangu tukio hilo lilipotokea, hawajaona polisi aliyefuatilia licha ya kutoa taarifa na kupewa fomu namba tatu iliyowezesha matibabu ya kiongozi huyo wa Chadema.

“Tunashangaa ni kwa nini polisi hawajatoa ushirikiano na huku taarifa wameshazipata,” alisema mmoja wa wakazi wa kijiji hicho ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Polisi anaswa akiwania uongozi UVCCM
Lilian Lucas, Morogoro
JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma, linamshikilia askari wake, F 7961 PC Stanley Mdoe wa Kituo cha Polisi Mvomero kwa tuhuma za kujihusisha na masuala ya siasa na kushiriki katika kinyang’anyiro cha kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (Nec) kupitia kundi la vijana.

Askari huyo pia anatuhumiwa kutumia ubini wa jina la Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera kama baba yake.

Habari  zilizopatikana kutoka mjini Dodoma zinadai kuwa askari huyo aliyejitambulisha kuwa yeye ni mtoto wa mkuu huyo wa mkoa, akijitambulisha kwa jina la Stanley Bendera, alikamatwa juzi jioni wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), ukiwa unaendelea mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, askari huyo akiwa amevalia sare za chama hicho tangu siku ya kwanza ya mkutano huo alikuwa akiomba wajumbe wa mkutano huo wampigie kura katika nafasi ya ujumbe wa Nec kupitia Mkoa wa Morogoro akiwa na wapambe wake ambao wengi wao walitokea mkoani humo.

Ilidaiwa kuwa askari huyo alikuwa amepamba gari lake kwa picha zake zilizokuwa zimeandikwa Stanley Joel Bendera jambo lililosababisha baadhi ya wanachama wa chama hicho wanaomfahamu kutoa taarifa kwa maofisa usalama waliokuwapo eneo hilo na Polisi Mkoa Dodoma ambao waliweka mtego wa kumkamata.
Mbali ya kukamatwa, askari huyo hakushinda katika nafasi hiyo. Awali, ilidaiwa kuwa askari huyo aliomba likizo isiyokuwa na malipo ili kupata fursa ya kushiriki uchaguzi huo.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alisema: “Sina taarifa ya askari huyo kujihusisha na siasa.”

Hata hivyo, Shilogile alisema alipata taarifa za kukamatwa kwake huko Dodoma akisema hata yeye alikuwa akimtafuta kwa shughuli za kikazi kwa siku mbili bila mafanikio.

Kamanda huyo alisema hana uhakika kuwa askari huyo amejiingiza katika siasa na kwa sasa ametuma askari wengine kufanya uchunguzi wa suala hilo.

Alisema endapo atabainika kujihusisha na siasa, atachukuliwa hatua za kinidhamu kulingana na taratibu za kijeshi.
Alisema endapo atathibitika kujihusisha na siasa, atakuwa amekiuka Katiba ya Tanzania Sura ya 9 inayokataza askari wa majeshi yote Tanzania kujihusisha na masuala ya siasa.

“Ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujihusisha na masuala ya siasa na kwamba kama ni kweli amefanya hivyo ni kinyume na kanuni na taratibu za kazi,” alisema Shilogile.

Ndege ya jeshi yaanguka, rubani afariki dunia
Waandishi Wetu
ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kapteni  Deogratius Magushi amefariki dunia na mwenzake Kapteni Feruz Kwibika kujeruhiwa vibaya wakati wakijaribu kujiokoa baada ya ndege waliyokuwa wakifanyia mafunzo kupata hitilafu ikiwa angani na kuanguka.

Ndege hiyo ilipata hitilafu jana saa 4.28 asubuhi katika Kambi ya Jeshi la Anga (Air Wing) Ukonga, Dar es Salaam.
Mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio, walisema ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa na kupoteza mwelekeo kabla ya kuanguka.

Msemaji wa Jeshi hilo, Kanali Kapambala Mgawe alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi, Lugalo.

Kanali Mgawe alisema Kapteni Kwibika aliumia vibaya kichwani na amelazwa katika Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU), hospitalini hapo.

Alisema kabla ya tukio hilo, marubani hao walikuwa wakijiandaa kurusha ndege hiyo mpya ya mafunzo lakini ikapata hitilafu wakati ikianza kushika kasi.

“Ilishindwa kuruka na ilitakiwa kuanguka katika hanga dogo ambalo lilikuwa na ndege nyingine. Ingekuwa ni hatari zaidi na pengine ingeleta maafa zaidi.”

Kanali Mgawe alisema baada ya marubani hao kuona hatari hiyo, waliamua kuirusha ndege hiyo umbali wa mita 100   hivyo wakapata wasaa wa kutumia parachuti.

Alisema baada ya kutoka katika parachuti hizo Kapteni Mangushi alianguka katika hanga dogo na kufariki papo hapo wakati Kapteni Kwibika aliangukia paa la nyumba na baadaye kuporomoka katika kambi na kuumia kichwa.
“Parachuti la Kapteni Kwibika lilikosa kizuizi na hiyo ndiyo ikawa sababu kubwa ya kuumia kwake,” alisema.

Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange alikuwa mmoja wa viongozi waliofika kushuhudia tukio hilo muda mfupi baada ya kutokea kwake.

Hata hivyo, Jenerali Mwamunyange hakuzungumza lolote kuhusiana na ajali hiyo.
Habari zilizopatikana jana jioni zinasema kuwa, ndege hiyo ilipangiwa safari ya kwenda katika Kambi ya Ngerengere Mkoa wa Morogoro na kurudi ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa askari hao.

Itakumbukwa kuwa, Juni 30, 2010 ndege nyingine ya JWTZ ya Kambi ya Ngerengere ilianguka katika eneo la Manga -Kabuku Mkoa wa Tanga.

Ndege hiyo iliyokuwa katika mazoezi ya vitendo, ilipata hitilafu hivyo kutua kwa dharura barabarani na kugongana uso kwa uso na basi lililokuwa limebeba watalii.

Ilielezwa kuwa, ndege hiyo ilikuwa imebeba watu watatu, wawili kati yao wakiwa ni marubani na mmoja wao alifariki dunia papo hapo.

Iliripotiwa kuwa hakuna abiria yeyote katika basi hilo la utalii aliyepoteza uhai. Hata hivyo, ndege hiyo ilisababisha kukwama kwa usafiri kwa abiria waliokuwa wanatoka na kuingia kwa kutumia barabara hiyo inayounganisha Mikoa ya Kaskazini na ile ya Pwani na nchi jirani.

Habari hii imeandikwa na Florence Majani, Ibrahim Yamola na Patricia Kimelemeta

UVCCM wapuuza agizo la JK
Waandishi Wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete jana alifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa chama hicho (UVCCM), huku akiwaambia kwamba “watajuta”, ikiwa watachagua viongozi kwa misingi ya rushwa.

“Nawaambieni, mkifanya mchezo ipo siku mtakuja kujuta maana mkishamchagua kiongozi asiyefaa, mtalazimika kuwa naye huyohuyo hadi 2017, na kama Waswahili wanavyosema majuto ni mjukuu,” alisema Rais Kikwete.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete ni kama aliyoitoa Jumapili usiku wakati akiahirisha mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wanawake ya chama hicho (UWT) pale aliposema CCM kinakwenda kubaya kutokana na chaguzi zake kugubikwa na vitendo vya rushwa.

Katika hotuba yake hiyo ya Jumapili, Rais Kikwete alisema siku zilizopita vitendo hivyo vilikuwa vikihusishwa zaidi na wanaume, lakini akaeleza kushangazwa kwake na makundi ya kina mama nao kuanza kujihusisha na rushwa.
Hata hivyo, kauli hizo za Rais Kikwete zilianza kupuuzwa usiku wa kuamkia jana kutokana na madai ya kushamiri kwa vitendo hivyo vya rushwa miongoni mwa wajumbe.

Vitendo hivyo vya rushwa vinadaiwa kutolewa na makundi ya wanasiasa wanaotafuta kuungwa mkono ndani ya CCM katika kinyang’anyiro cha urais kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa 2015.

Waandishi wetu ambao walitembelea sehemu mbalimbali hasa hoteli na nyumba za kulala wageni kati ya saa nne usiku na tisa alfajiri, walishuhudia harakati za kutoa na kupokea fedha ili kushawishi wajumbe kuwapigia kura wagombea wanaowataka.

Usiku wa saa 7:30, mmoja wa makada wa CCM alimwambia mwandishi wetu kwamba kuna fedha nyingi zimemwagwa katika uchaguzi huo na kwamba hata vyombo vya usalama kama Polisi, Usalama wa Taifa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ni kama havipo.

“Kama hata ninyi waandishi wa habari mnashindwa kuandika haya tunayoyaona usiku huu, basi nchi hii inakwenda pabaya sana. Maana nyie ndiyo mliobaki na hakuna mtetezi wetu mwingine. Chama chetu kimekuwa cha ajabu sana, hakuna jinsi unaweza kupata uongozi bila fedha,” alisema.

Baadhi ya wajumbe walidai kwamba kulikuwa na gari ambalo lilikuwa likizunguka na kiasi kikubwa cha fedha ambazo zilikuwa zikigawanywa kwa wajumbe katika hoteli na nyumba za kulala wageni walikofikia.

Katika kufuatiliana, takriban saa 8.30 usiku, magari ya kambi tofauti yalionekana yakikimbizana katika eneo la Area ‘C’, baada ya wajumbe wa kambi moja kuwahisi wenzao kwamba walikuwa wakigawa fedha hivyo kutaka kuwakamata.

Ulikuwa ni kama mchezo wa kuigiza kwani wakati mwingine, magari yalikuwa yakikutana katika makazi ya wajumbe na ilipotokea hivyo yote yalisita kusimama na badala yake yaliendelea na safari na baadaye kurejea.

Kulikuwa na taarifa kwamba wajumbe wa mkutano huo kutoka Tanzania Zanzibar walihamishwa kwa muda usiku baada ya kupewa fedha na kambi mojawapo, kwa lengo la kuhofia kwamba kambi nyingine ingewabadilisha mawazo.

Mkakati pia unadaiwa kusukwa kuwahamisha wajumbe wa Mikoa ya Mbeya na Singida kwa nyakati tofauti, lakini jaribio hilo liligonga mwamba kutokana na wajumbe hao kukataa kwamba ulikuwa ni usumbufu kutokana na kuchoka kwa safari ndefu.

Katika moja ya hoteli zilizopo Area ‘C’, mwandishi wetu alishuhudia baadhi ya wajumbe kutoka mikoa kadhaa wakiingia hotelini hapo saa 7:15 usiku na baada ya dakika kama 10 hivi, waliingizwa kwenye chumba maalumu ambako walikaa kwa zaidi ya saa nzima.

Saa 7:54 usiku, umeme ulikatika Mji mzima wa Dodoma na ulirejeshwa saa 8.08, tukio ambalo baadhi ya wajumbe walidai kwamba huenda ulikuwa mpango wa kufanikisha kugawa fedha katika baadhi ya maeneo yaliyokuwa yakihofiwa kutokuwa na usalama.

Uchaguzi wa UVCCM kwa ujumla wake umevuta makada wengi wa chama hicho wakiwamo mawaziri na wabunge ambao walikuwa washiriki rasmi wa kampeni hizo za usiku wa kuamkia jana.

Kauli ya Kikwete
Rais Kikwete wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane wa UVCCM jana, alikiri kuwa mwelekeo wa CCM si mzuri hivyo akawaomba vijana “kukinusuru chama chao”.

Alisema watu wamekuwa wakikisema vibaya jambo linalomfanya aone kuwa umefika wakati ya kuwapo mabadiliko.
“Chama chetu kinasemwa vibaya kila mahali kwamba sisi lazima mtu aununue uongozi kwa fedha na kwamba kura zinanunuliwa, hivi jamani sisi tunakwenda wapi, vijana lazima mbadilike,” alisema Kikwete na kuongeza:
“Nayasema haya kwa dhati ya moyoni kuwa ni lazima tubadilike na umefika wakati sasa ambao kila mmoja wetu afanye mabadiliko na mabadiliko lazima yaanzie kwenu vijana.”

Rais aliwaagiza vijana kutumia Ibara ya Tano ya Katiba yao ambayo inaelekeza kuwa nia ya CCM ni kuhakikisha kuwa chama kinabaki madarakani wakati wote bila ya kuyumba.

Alisema kuwa vijana hao wakijipanga wanaweza kukisaidia CCM kuendelea kubaki madarakani kizazi hadi kizazi na nchi wakati wote itakuwa chini ya chama hicho.

Alisema CCM si chama cha michezo, kama mpira wa miguu, bali ni chama cha siasa ambacho kinapaswa kuwa makini wakati wote.

Awali, akimkaribisha Rais Kikwete, Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa alikiri kuwa wakati mwingine vijana walikuwa wakikimbia mwendo mrefu kiasi cha kukwazana na chama.

Malisa alimpongeza Rais Kikwete kwa kuwa mvumilivu katika yote akisema kama angeamua kusimama katika haki, ni wazi kuwa hata yeye (Malisa) asingekuwa katika nafsi hiyo.

Mwenyekiti huo alijivunia mafanikio kuwa amemaliza kuongoza umoja huo akiacha ujenzi wa jengo la kitega uchumi la ghorofa 16.

Ushindani mkubwa
Makundi ya vijana yalianza kujikusanya nje ya Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma jana saa mbili asubuhi, huku yale yaliyokuwa yakiwaunga mkono baadhi ya wagombea yakiimba nyimbo za hamasa yakiwa yamebeba picha za wagombea husika.

Wakati huo ulinzi uliimarishwa kwani gari la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) likiwa na askari wapatao 12 lilikuwa likizunguka eneo hilo na baadaye kuegeshwa mbele ya ukumbi huo.

Kazi kubwa ilikuwa ni ya kugawa mamia ya vipeperushi vyenye wasifu wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi, ambayo kwa kiasi kikubwa ilifanywa na wapambe wa wagombea husika wakisaidiwa na baadhi ya makada wa CCM wa mjini Dodoma.

Mmoja wa makada hao (jina tunalihifadhi kwa sasa) alisema kazi hiyo ilikuwa ikifanywa kwa ujira kati ya Sh10,000 na 20,000.

Vita kubwa katika uchaguzi huo ni katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti iliyokuwa ikiwaniwa na Paul Makonda, Mboni Mhita na Ally Salum Hapi, wakati nafasi ya Mwenyekiti ni Sadifa Juma Khamis, Rashid Simai Msaraka na Lulu Msham Abdallah.

Hadi tunakwenda mitamboni jana jioni, Sadifa Juma Khamis alishinda nafasi ya Uenyekiti wakati kwa upande wa Makamu Mwenyekiti Mboni Mhita alikosa kura 30 kufika nusu ya kura zote zilizopigwa na Paul Makonda alishika nafasi ya pili.

Kutokana na matokeo hayo, uchaguzi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa ilibidi urudiwe ili kupata mshindi kwa nusu ya kura zote.

Kenyatta aomba msaada wa Kikwete urais Kenya
Waandishi Wetu Dar, Nairobi

KESI inayowakabili Wakenya wanne kuhusu vurugu za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2008 iliyopo katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), imechukua sura mpya baada ya mmoja wa watuhumiwa hao, Uhuru Kenyatta kwenda na ujumbe wake kwa Rais Jakaya Kikwete kumwomba amuunge mkono katika harakati zake za urais.

Kwa mujibu wa gazeti la Standard la Kenya, Rais Kikwete alikutana na kiongozi huyo wa Chama cha The National Alliance Ikulu na kufanya naye mazungumzo yaliyodumu kwa saa tatu.

Katika kikao hicho pia kulikuwa na wajumbe wengine kutoka chama cha URP cha William Ruto na wale wa New Ford Kenya wakiongozwa na Waziri wa Sheria, Eugine Wamalwa anayetajwa kuwa mgombea mwenza wake.

“Kenyatta alisema kuwa malengo yake na viongozi wenzake ni kuipeleka Kenya mbele wakiwa na umoja. Kwa kumalizia akasema, wanalenga kuwafikia viongozi wa vyama vya siasa,” alisema Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kenyatta, Munyori Buku.

Ujumbe wa Uhuru umekuja ikiwa ni siku moja kabla ya kuwasili Nairobi kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa  ICC, Fatou Bensouda kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo na kujionea maeneo yaliyoathiriwa na vurugu hizo.

Umuhimu wa safari hiyo pia umetokana na safari ya Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan na Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa nchini Kenya hivi karibuni, huku wakiwa na ujumbe kwamba Kenyatta na Ruto hawana sifa mbele ya Wakenya na jumuiya ya kimataifa ya kugombea urais.

Annan ndiye aliyesimamia mchakato wa amani katika kazi ambayo alisaidiana na Rais Kikwete na Mkapa.

Annan na Mkapa inasemekana walikwenda Nairobi na kufanya majadiliano na Rais Mwai Kibaki yanayoaminika kujikita katika kesi hiyo ya ICC sanjari na Uchaguzi Mkuu wa Machi 4, 2013.

Inaaminika kuwa ujumbe huo kutoka Kenya ulikuja makusudi kwa Rais Kikwete hasa kwa kuwa ana uhusiano mzuri na viongozi wakubwa wa mataifa ya Magharibi akiwa pia amechangia katika kuleta amani nchini humo baada ya vurugu za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2008.

Hivyo wamelenga kumtuma Rais Kikwete kupeleka ujumbe ICC ili kuwaruhusu wagombee katika Uchaguzi Mkuu kwa manufaa ya uchaguzi wa amani na Kenya kwa jumla.

Katika ziara yake, Annan alikaririwa akisema: “Ni kweli kuna mambo ambayo kila mtu angependa yaangaliwe hasa kwa watu wanaotajwa kugombea urais.”

Kauli hiyo imewatisha Uhuru na Ruto ambao walilipuka wakimtaka Annan kuachana na mambo ya Kenya.

Kuhusu hilo Buku alisema: “Wakenya ndiyo waamuzi wa hatima yao … Rais Kikwete ameombwa kushawishi kuheshimiwa kwa uamuzi wa Wakenya. Ndiyo waamuzi wa hatima yao hivyo ni lazima waruhusiwe kuchagua viongozi wao bila kuingiliwa. Rais amegusia kwamba, Afrika ingeheshimu uamuzi, Wakenya wangefanikisha uchaguzi mkuu wa Machi mwakani.

“Hatuna matatizo na marafiki zetu, lakini kama hawatuheshimu hilo ni shauri yao, tuna marafiki wengi wa kufanya nao kazi ulimwenguni kote,” alisema Uhuru wiki iliyopita jijini Nairobi.

Akiwa nchini, inasemekana kuwa Uhuru alikuwa akirudia maoni yake kwa Rais Kikwete kwamba ni makosa kwa wageni kuingilia uchaguzi wa Kenya.

Katika hatua nyingine, mwandishi wa Mwananchi alimshuhudia Kenyatta akiwa katika Mgahawa wa Rose Garden, Dar es Salaam akipata vinywaji na nyama choma.

Baada ya kuingia Rose Garden akiongozana na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mutinda Mutiso, wateja na watu mbalimbali walikwenda kumsalimia mtoto huyo wa Rais wa Kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta ambaye alionekana mwenye furaha na hakukuwa na ulinzi mkubwa.

Madabida: Tunaendelea kuzalisha ARV
Pamela Chilongola

UONGOZI wa kiwanda cha kutengeneza dawa za kupunguza makali ya Ugonjwa wa Ukimwi (ARV) cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited (TPI), umesema hautasitisha uzalishaji wa dawa hizo kwa kuwa hauna barua inayowakataza kufanya hivyo kutoka mamlaka yoyote.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku 12 baada ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi kutangaza kufungia uzalishaji wa dawa hizo katika kiwanda hicho.

Mkurugenzi Mkuu wa TPI, Ramadhani Madabida alisema jana kwamba kiwanda hicho bado kinaendelea kuzalisha dawa hizo kwa kuwa hakuna barua kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyowataka wasimamishe uzalishaji huo.

“Wenye mamlaka ya kukifungia kiwanda chochote cha dawa na kukithibitisha ni TFDA (Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania),siyo Wizara ya afya,” alisema.

Alisema baada ya tukio hilo, TFDA iliwataka kwa barua, watoe maelezo ndani ya siku 14 kuhusu mzunguko wa dawa hizo na siyo kusitisha uzalishaji... “Sisi tuliletewa barua na TFDA ambayo ilitutaka tutoe maelezo ndani ya siku 14 kuhusu dawa feki za ARV zilizosambazwa na kudaiwa kuwa ni za kwetu na tuliwaeleza.”

Alisema walifanya hivyo kwa wakati na TFDA iliwahakikishia na kuwathibitishia kuwa hizo dawa hazikutengenezwa katika kiwanda hicho.

“Sisi hatuna uwezo wa uelewa wa utengenezaji wa dawa za ARV bandia zilizokutwa katika mzunguko, wenyewe wanajua zilipotengenezwa na si hapa, ni nje ya nchi na wanafahamu kinachoendelea,” alisema Madabida.

Alisema kiwanda hicho kinazalisha dawa hizo kama kawaida na hawana kitu cha kuwakwaza kutoendelea na uzalishaji.

Alisema wanatarajia kuongeza uzalishaji kwa asilimia 70 na Desemba mwaka huu wanatarajia kuzindua kiwanda kipya ambacho kitakuwa kikifanya kazi chini ya Shirika la Afya Duniani (WHO) na kitakapokamilika, kitakuwa na uwezo wa kuuza dawa hizo ndani na nje ya Tanzania.

Pia alisema wanachukua hatua zao na kuhakikisha umma  unaelezwa ukweli wa dawa za ARV bandia zilipopatikana.

Hata hivyo, kauli ya Madabida ilipingwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Donald Mmbando aliyesema jana kuwa kiwanda hicho kilipelekewa barua ya kujieleza na kusitisha uzalishaji ndani ya siku 14.

“Tuliletewa nakala ya barua kutoka TFDA ambayo wamemwandikia mmiliki wa kiwanda cha TPI kuwa atoe maelezo ndani ya siku 14 na kusitisha uzalishaji wa dawa hizo… Mmiliki anavyodai hajapewa barua, si kweli,” alisema Dk Mmbando.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA, Dk Hiiti Silo na Ofisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Gaudensia Simwanza hawakupatikana jana kutoa ufafanuzi juu ya sakata hilo baada ya simu zao kutopatikana.

Hatua ya TPI kutakiwa kusimamisha uzalishaji wa dawa hizo, ni baada ya kubainika kuwapo kwa dawa bandia katika mzunguko zenye alama ya biashara, TT-VR 30 toleo namba OC.01.85 mwanzoni mwa Septemba mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime baada ya TFDA kufanya ukaguzi.

Akitangaza hatua ya kukifungia kiwanda hicho, Dk Mwinyi alisema baada ya kufanya uchunguzi, walibaini kuwa nyaraka zinaonyesha kuwa TPI ndicho kilichoiuzia MSD ARV bandia.

“Wamesimamishwa ili kupisha uchunguzi kwa sababu wanatakiwa kufanya uchunguzi wa kile wanachokipokea… Tunachoona hapa ni kwamba uchunguzi haukufanyika sawasawa ndiyo maana tumechukua hatua za kuwasimamisha,” alisema Dk Mwinyi alipokuwa akizungumza Dar es Salaam na kuongeza:

“Matumizi ya dawa hiyo inayotengenezwa na TPI yamesimamishwa na imeondolewa katika vituo vya kutolea huduma za afya na kurudishwa MSD,” alisema.

Alisema tayari makopo 9,570 ya dawa hiyo yamerejeshwa MSD na kwamba bado makopo mengine 2,600 yapo katika utaratibu wa kukusanywa.

Waziri huyo alisema dawa hiyo ilitengenezwa Machi mwaka huu na muda wa matumizi yake unatarajiwa kumalizika Februari mwakani huku zikiwa na rangi mbili tofauti, njano na nyeupe.

Alisema dawa zilizokuwa na rangi ya njano zilikuwa na kiambata cha Efaverenz badala ya viambata aina ya Niverapine, Lamivudine na Stavudine vilivyopaswa kuwapo.

Dk Mwinyi alisema vidonge vilivyokutwa kwenye vifungashio vya dawa husika vilikuwa tofauti na vifungashio vilivyosajiliwa na TDFA.

Kesi ya Makunga yaanza kunguruma
Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Msaidizi anayesajili Magazeti, Rafael Hokororo (57) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa waraka uliondikwa na Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Samson Mwigamba ulikuwa unashawishi askari wagome na wasipokee amri kutoka kwa wakuu wao.

Hokororo aliitoa ushahidi wake jana kwenye kesi inayomkabili aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Theophil Makunga na wenzake.Akitoa ushahidi katika kesi hiyo,  Hokororo alidai Novemba 30, 2011 akiwa ofisini kwake Dar es Salaam, anakumbuka alipokea magazeti mengi likiwamo gazeti la Tanzania Daima.

Shahidi huyo wa upande wa mashtaka alidai kuwa, siku hiyo alisoma makala imeandikwa ‘Waraka maalum kwa askari wote’, iliyoandikwa kwenye safu ya Kalamu ya Mwigamba na mwandishi Samson Mwigamba.
Alidai kuwa: “Tulisoma walaka huo  na tukajiuliza hii ni maoni, barua ama wito. Lakini tuliona ni maalumu kwa Jeshi la JW, Magereza na Polisi.”

Baada ya kueleza hayo, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Prosper Mwangamila alimhoji shahidi huyo kuwa walibaini nini?

Shahidi huyo akijibu alidai kuwa, lugha iliyotumiwa ilikuwa siyo nzuri na kwamba ilikuwa inawashawishi askari wagome, wasipokee amri kutoka kwa wakuu wao.

Pia, aliulizwa iwapo akiona nakala ya gazeti hilo atalikumbuka huku  akimuonyesha.Hokororo alidai ataikumbuka na kwamba waraka huo uliandikwa kwenye ukurasa wa 14 wa gazeti la Jumatano la Novemba 2011 na kuomba mahakama kulitoa kama kielelezo cha ushahidi.

Wakili wa utetezi, Isaya Matambo alipinga akiiomba mahakama isipokee nakala hiyo ya gazeti kama kielelezo cha ushahidi kwa sababu nakala hiyo haionyeshi sifa ya kuwa gazeti na kwamba, halijulikani ni gazeti gani.

Wakili mwingine wa utetezi, Gabriel Mnyele alimuunga mkono wakili Matambo na kuongeza kuwa nakala iliyowasilishwa na upande wa mashtaka mahakamani hapo  haijakamilika.

Baada ya kutolewa kwa pingamizi hayo, Wakili Mwangamila aliliondoa ombi la kuwasilisha nakala ya gazeti hilo kama kielelezo cha ushahidi katika kesi hiyo.

Hakimu Lema aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 7, mwaka huu.
Katika kesi hiyo, Makunga anakabiliwa na shtaka  la kuchapisha makala ya  kuwashawishi askari na maofisa wa majeshi nchini kuacha kuitii Serikali.

Washtakiwa wengine ni Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absolum Kibanda. Wanatetewa na mawakili, Deo Ringia, Isaya Matambo, Juvenalis Ngowi na Nyoronyo Kicheere.

Jalada la Lulu larejeshwa Kisutu
Tausi Ally
MSANII  wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji, amehoji Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu lilikofikia jalada la kesi.

Lulu aliuliza swali hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Stuarti Sanga baada ya Wakili wa Serikali, Keneth Sekwao kudai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba, upelelezi wake haujakamilika.

Baada ya Sekwao kueleza hiyo, Lulu alinyoosha mkono na kuhoji jalada la kesi inayomkabili lilikofikia.
Hakimu Sanga alimuuliza Wakili Sekwao iwapo anauliza jalada halisi au la kudurufu.

Wakili Sekwao alimwambia Hakimu Sanga kuwa, anaulizia jalada halisi.Hakimu Sanga alimwambia Lulu kuwa jalada halisi limekwisharudi  na kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 5, mwaka huu itakapotajwa tena.

Lulu anatuhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba. Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwa Kanumba, Sinza, Dar es Salaam.